Header Ads

Responsive Ads Here

KAMATI YA BUNGE KUTOKA MALAWI WAZURU MLIMA RUNGWE


1Baadhi ya Wabunge wa Kamati ya Maliasili na Mabadiliko ya tabia ya nchi kutoka nchini Malawi wakiwa wanapumzika jana  mara baada ya kupanda Mlima Rungwe  mpaka kituo cha kwanza cha mapumziko  lengo la ziara hiyo ikiwa ni  kujifunza  jinsi  Wakala wa Huduma Misitu Tanzania (TFS) wanavyofanya  suala la  uhifadhi kwa kuwashirikisha wananchikatika kuzilinda hifadhi hizo.

2
Baadhi ya Wabunge wa Kamati ya Maliasili na Mabadiliko ya tabia ya nchi kutoka nchini Malawi wakiwa wanapanda jana Mlima Rungwe ambapo waliweza kupanda mlima huo  mpaka kituo cha kwanza cha mapumziko
3Afisa Misitu, Anna Lauo akifanya mahojiano jana na mwandishi wa habari katika eneo la Mlima Rungwe
4Mwenyekiti wa kamati ya Maliasili na Mabadilik ya tabia nchi, Welani Chilenga akizungumza na vyombo vya habari mara baada kupanda Mlima Rungwe  mpaka kituo cha kwanza cha mapumziko.
…………………………………………………………..
Wabunge wa Kamati ya Maliasili na Mabadiliko ya tabia ya nchi kutoka nchini Malawi wamefanya ziara ya mafunzo kwenye Msitu wa asili wa Hifadhi  wa Mlima Rungwe mkoani Mbeya na kujionea jinsi wananchi wanavyoshirikishwa katika uhifadhi wa pamoja.
Akizungumza  Mwenyekiti wa kamati hiyo, Welani Chilenga amesema lengo la ziara hiyo ni kutaka kujifunza  jinsi  Wakala wa Huduma Misitu Tanzania (TFS) wanavyofanya   uhifadhi kwa kuwashirikisha wananchi katika kuzilinda hifadhi zao.
Amesema nchini Malawi wao wamekuwa wakitumia mitutu katika kulinda Misitu jambo ambalo halijawawezesha kufanikiwa katika uhifadhi hivyo sehemu kubwa ya miti yao imekatwa.
Chilenga  amesema wamejionea vyanzo vya maji ambapo mlima huwa ni chanzo cha mito 21 na wameiomba TFS kuendelea na juhudi za uhifadhi kwani nao wamekuwa wakifaidika na Mlima huo kama chanzo chao cha maji kupitia ziwa Nyasa
Katika hatu nyingine, Wabunge wa Kamati hiyo walifanikiwa kupanda mlima huo mpaka kituo cha kwanza cha mapumziko.
Awali, Mhifadhi Mkuu wa Mlima Rungwe, Innocent Lupembe amewataka watanzania kutembelea hifadhi hiyo ili waweze vivutio mbalimbali vinavyopatikana katika hifadhi hiyo wakiwemo ndege na wanyama wa aina mbali mbali.
Aidha, Aliwataka watafiti wa ndani na nje ya nchi wafanye tafiti katika hifadhi hiyo kwa kuwa ina amali ambayo haipatikani mahali popote pale duniani nisipokwa katika Mlima huo.

No comments