Header Ads

Responsive Ads Here

“JUNDOKAN TANZANIA – GOJU RYU KARATE-DO”KUPANDISHA NGAZI WANAFUNZI WA DOJO DAR


Sensei Rumadha Fundi mtaalam Karate anayetambuliwa na baraza la mchezo huo lenye makao Okinawa-Japan
Mtindo wa karate mkongwe  duniani, Okinawa Goju Ryu wa chama cha  Jundokan  Tanzania chini ya mwakilishi wake Sensei Rumadha Fundi  mwenye Dan 4,“Yondan” pia mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 38 ya mafunzo ya sanaa ya Karate mtindo wa Goju Ryu chini ya walimu wakuu wengi maarufu toka Okinawa, Japan kama vile Master Mario Higaonna(IOGKF), Master Masataka Muramatsu( Goju Ryu Kyokai), Teruo Chinen( Jundokan International), na hatimae Kancho Yoshihiro Miyazato, mwenyekiti wa (Jundokan So Honbu, Naha, Okinawa)Master Tetsunosuke Yasuda, Master Tsuneo Kinjo na Master Tetsu  Gima.

Tunatarajia kufanya mitihani ya mikanda mieusi miezi ijayo madaraja tofauti kupitia dojo za “ Kaizen dojo” Jamhuri na dojo dada ya Hekalu la Kujilinda Zanaki dojo. Hii ni moja ya jitihada za kusambaza mwenendo huu kwa kina na pia ufundishaji wa mbinu za utumiaji wa tafsiri za “Kata” uijulikanao kama “Bunkai”, au uchambuzi wa matumizi ya mbinu za kujilinda. Mitihani yote itafanywa na sensei Rumadha Fundi chini ya utaratibu wa “Syllabus”  ya Jundokan, Okinawa.
Lengo pia ni kuzungumzia yale yote yaliojiri katika semina kuu ya Jundokan bara la Ulaya chini ya master wake toka jijini Naha, Okinawa mwezi wa Julai 2017. Ufundishaji sahihi wa mfumo huu ni moja ya malengo kuhakikisha tu kwamba wana Jundokan duniani mkote wapo kwenye msimamo mmoja katika uchambuzi na ufanyaji wao wa Kata na matumizi yake.
Pia wakati huohuo, kutakuwa na semina ya wanafunzi wa ngazi za mikanda mieusi wa Jundokan Tanzania ikiwemo na dojo ya Zanaki katika kuwawezesha wanafunzi wake kuuliza na kupata majibu ya matumizi yao ya ufanyaji Kata kama jinsi ipasavyo chini ya chama hicho chenye ufahasa wa mtindo huo unaofuata nyanyo za mafunzo ya Master Chojun Miyagi, mwanzilishi wa mtindo wa Okinawa Goju Ryu.
Hivyo, hii ni moja ya fursa kubwa kwa wana Jundokan kuweza kushiriki semina hii chini ya mwakilishi wa Jundokan Tanzania, ama kamaijulikanavyo “Tanzania Shibu-Cho”, sensei Rumadha Fundi. Sensei Rumadha, amesisitiza kwa niaba ya chama hicho kwamba Kila mwanafunzi wa mkanda mweusi, hana budi kuhudhuria semina za walimu angalau mara moja kila miaka miwili na kupata usahihisho muhimu kimafunzo. Hilo ndio lengo kuu hata kipindi kile kwa mwanzilishi wa Okinawa Goju Ryu Tanzania, marehemu Sensei NC Bomani kufanya ziara za mara kwa mara kwenda huko Naha, Okinawa kupata marekebisho toka kwa magwiji wa Karate duniani na chimbuko lake.
Pia vilevile, Tanzania imepatiwa mwaliko wa kuhudhuria maadhimisho ya miaka 65 tokea kuanzishwa kwa chama cha Jundokan itayofanyika November 2018 mjini Naha, Okinawa, Japan. Chama hicho kilianzishwa na mwanafunzi mkuu wa Master Miyagi aitwae Master Eiichi Miyazato sensei 1957 ambae pia alikuwa ndio mwalimu wa sensei Nantambu C Bomani. “ Chuo kinacho fundisha nyayo au mwenendo wa Master Chojun Miyagi”. Ikimaanisha, hamna mabadiliko yeyote kimafunzo na Kata zake kama jinsi alivyokuwa akifundisha mwanzilishi wake Chojun Miyagi sensei.

No comments