Header Ads

Responsive Ads Here

IGP SIRRO AWASILI NCHINI AKITOKEA RWANDA


Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, amewasili nchini akitokea nchi ya Rwanda, alipokwenda kwa ajili ya ziara ya kikazi ambapo akiwa nchini huko alipokelewa na mwenyeji wake IGP wa Rwanda Emmanuel Gassana.

Katika ziara hiyo yenye lengo la kubadilishana uzoefu na namna ya kukabiliana na uhalifu unaovuka mipaka, biashara ya dawa za kulevya usafirishaji wa binadamu ikiwa pamojana kufanya operesheni za pamoja.
Aidha, IGP Sirro, amelialika Jeshi la Polisi Rwanda kuja nchini kujifunza na kufanya mazoezi ya pamoja  ya kijeshi.

No comments