Header Ads

Responsive Ads Here

DKT. PALLANGYO AONGOZA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA BAJETI ZIARA KATIKA MIRADI YA GESI LINDI


PICHA NA 1
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (katikati) akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Hai, Freeman Mbowe ambaye ni mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, mara baada ya kuwasili katika eneo la Kiwanda cha Kuzalisha vigae (tiles) cha Goodwill Ceramic kilichopo Mkuranga kwa ajili ya kuanza ziara hiyo

PICHA NA 2
Msimamizi wa Uzalishaji na Ujenzi katika Kiwanda cha Kuzalisha vigae (tiles) cha Goodwill Ceramic kilichopo Mkuranga mkoani Pwani,  Said Ngongoki akielezea jinsi uzalishaji  unavyofanyika kiwandani hapo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (katikati) pamoja na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti mara walipofanya ziara kiwandani hapo
PICHA NA 3
Meneja  Rasilimaliwatu kutoka katika Kiwanda cha Kuzalisha vigae (tiles) cha Goodwill Ceramic kilichopo Mkuranga mkoani Pwani, Msafiri Figa ( wa kwanza kulia) akitoa ufafanuzi  kwa  wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti katika eneo la uzalishaji la kiwanda hicho.
PICHA NA 4
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (katikati) akibadilishana mawazo na mwakilishi kutoka Idara ya Biashara katika Kiwanda cha Kuzalisha vigae (tiles) cha Goodwill Ceramic kilichopo Mkuranga mkoani Pwani, Emily Wu (kulia) katika eneo la uzalishaji la kiwanda hicho
PICHA NA 5
Mtaalam kutoka Shirika la Maendeleo  ya Petroli Nchini (TPDC), Dominick Ngunyali (kulia) akitoa ufafanuzi juu ya jinsi gesi inavyopokelewa katika Kiwanda cha Kuzalisha vigae (tiles) cha Goodwill Ceramic kilichopo Mkuranga mkoani Pwani kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti katika eneo la kupokelea gesi hiyo
PICHA NA 6
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (mbele kulia) akiongoza wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kwenye ziara katika eneo la Kiwanda cha Kuzalisha vigae (tiles) cha Goodwill Ceramic kilichopo Mkuranga mkoani Pwani.
PICHA NA 7
Meneja  Rasilimaliwatu kutoka katika Kiwanda cha Kuzalisha vigae (tiles) cha Goodwill Ceramic kilichopo Mkuranga mkoani Pwani, Msafiri Figa (kushoto) akielezea jinsi udongo wa aina mbalimbali unavyochanganywa katika hatua za awali za maandalizi ya utengenezaji wa vigae (tiles) kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti.
PICHA NA 8
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kulia) akitoa maelekezo  kwa Mhandisi wa Mitambo katika Kituo za  Kuzalisha Umeme kwa Kutumia  Gesi cha Somangafungu kilichopo mkoani Lindi, Edwin Konyani katika ziara hiyo.
PICHA NA 9
Msimamizi wa Bomba la Gesi  Upande wa Umeme  katika Kituo cha Kupokea Gesi kutoka  Songosongo na Madimba Joseph Msafiri (katikati) akielezea jinsi  gesi inavyopokelewa katika kituo hicho kwa  wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti katika ziara hiyo.
PICHA NA 10
Sehemu ya Kituo cha Kupokea Gesi kutoka  Songosongo na Madimba kilichopo Somangafungu mkoani Lindi.
…………………….
Leo  Agosti 22, 2017 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo ameongoza Kamati y Kudumu ya Bunge ya Bajeti katika maeneo mbalimbali yenye miradi ya gesi katika mkoa  wa Lindi lengo likiwa ni kuona utekelezaji wa miradi hiyo. Kati ya maeneo waliyotembelea ni pamoja na  Kiwanda cha Kuzalisha vigae (tiles) cha Goodwill Ceramic kilichopo Mkuranga mkoani Pwani,  Kituo cha Kuzalisha Umeme kwa kutumia  Gesi  Asilia cha Somangafungu,  Makutano ya Bomba la Gesi Asilia (Somangafungu) mkoani  Lindi pamoja na eneo linalotarajiwa kujengwa Mitambo ya Kuchakata na Kusindika  Gesi Asilia (LNG) lililoko katika Manispaa ya Lindi.

No comments