Header Ads

Responsive Ads Here

DKT. KALEMANI AENDELEA KUZINDUA MIRADI YA UMEME VIJIJINI AWAMU YA TATU (REA PHASE III MIKOA YA KUSINI NA RUKWA


Naibu Waziri Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani akiwasili eneo la uzinduzi Mkoani Rukwa, akiwa amepokelewa na mwenyeji wake Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mheshimiwa Saidi Mtanda.
 
Na Henry Kilasila – Rukwa

Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Dkt Medard Kalemani ameendelea na ziara za uzinduzi wa Miradi ya Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA PHASE III) ambapo Agosti 14, 2017 alikuwa Mikoani Rukwa katika Kijiji cha Kabwe Wilaya ya Nkasi.Dkt. Kalemani alisema jumla ya Shilingi Bilioni 42.5 zitatumika kupeleka umeme
katika Mkoa huo na kuongeza Mradi huo utatekelezwa katika vipindi viwili
tofauti ambapo sehemu ya kwanza itahusisha upelekaji umeme katika vijiji 111.”Sehemu ya pili itahusisha vijiji 145 ambapo itaanza baada ya
kukamilika  kwa sehemu ya kwanza. Kufikia mwaka 2021 vijiji vyote vya Mkoa
wa Rukwa vitakuwa vimepatiwa umeme”.Alisema Dk. Kalemani.
Aidha, Dkt. Kalemani alimtambulisha Mkandarasi atakayejenga Mradi wa REA
Mikoani humo Kampuni ya Kitanzania ya Nakuroi Investment Company Limited.
Alimwagiza Mkandarasi kuhakikisha anapeleka umeme Kijiji kwa Kijiji na
Kitongoji kwa Kitongoji bila kuruka na sehemu zinazotoa huduma za Kijamii kama
Mashule, Zahanati, Magereza, Visima vya maji, Nyumba za Ibada na sehemu
mbalimbali.
Pia alitoa maagizo kwa TANESCO kupeleka Ofisi katika Kijiji cha Kabwe na katika
maeneo yote yenye Wateja wengi lakini wapo mbali na Huduma za TANESCO.
Aliongeza kwa kuwataka Mameneja  na Watalaamu wa TANESCO kutokukaa Ofisini
bali wawafuate Wateja.
Awali, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji TANESCo, Dkt. Tito E. Mwinuka aliwaomba
Wananchi hao wa Kabwe kuwa waaminifu na kutoa ushirikiano kwa Watendaji wa
TANESCO kabla na hata baada ya Mradi kukamilika.
“Muitunze miundombinu ya umeme, msiihujum wala kuichoma moto”.
Alisema Dkt. Mwinuka.
Alisema TANESCO imejipanga kuhakikisha Wananchi hao wanapata huduma ya umeme
iliyobora na ya uhakika.
Mbunge wa Nkasi, Ali Kessy  aliwaeleza Wananchi kuwa mradi huo wa
usambazaji umeme vijijini hauna malipo ya fidia hivyo watoe ushirikiano kwa
wakandarasi hao wakati wanatekeleza mradi huo.
Mkuu wa Wilaya ya Nkansi Mheshimiwa Saidi Mtanda aliushukuru Uongozi wa TANESCO
kwa kwani umekuwa ukitoa ushirikiano pale unapohitajika.
“Mheshimiwa Mgeni Rasmi katika Kijiji cha Nyamare kwenye chanzo cha maji
tulileta Mkandarasi akatukadilia bei ya Transifoma milioni 60, tuliwasiliana na
uongozi wa TANESCO wametufungia Transfoma kwa pesa zao milioni 24”.
Alisema Mheshimiwa Mtanda.
Mheshimiwa
Naibu Waziri wa
Nishati na Madini,Dkt Medard Kalemani alimalizia uzinduzi Mkoani Rukwa kwa kuwakabidhi Wazee kumi zawadi ya kifaa cha UMETA.
 Naibu waziri Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Dkt Medard Kalemani akifurahia baada
ya kuzindua mradi wa REA RUKWA

Kutoka kushoto Mkurugenzi Mkuu REA, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji TANESCO
Dkt. TITO E. Mwinuka katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Kampuni ya
Nakuro
Investment Company Limited inayojenga Mradi huo wa umeme Mkoani humo.
Naibu waziri Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Dkt Medard Kalemani akipata
maelezo ya namna kifaa cha UMETA kinavyofanya kazi kutoka kwa Bw. Lucas Kusare Afisa Huduma kwa Wateja Mkoa wa RukwaNo comments