Header Ads

Responsive Ads Here

DC KISHAPU MHE.TARABA AMESEMA ZOEZI LA UTAMBUZI,USAJILI NA UFUATILIAJI WA NG’OMBE KWA KUTUMIA CHAPA LITAPUNGUZA CHANGAMOTO KWA WAFUGAJI


1
Mkuu wa wilaya ya Kishapu, Mheshimiwa Nyabaganga Taraba akizungumza katika kikao cha kuhamasisha utambuzi, usajili na upigaji chapa kwa maofisa mifugo na watendaji kata na vijiji (hawapo pichani).

2
Ofisa Mifugo anayeshughulikia afya na tiba, Farles Mwenura akionesha kifaa maalumu cha kupigia chapa ng’ombe kwa maofisa mifugo na watendaji kata na vijiji wakati wa kikao hicho.
3
Maofisa mifugo kata, watendaji kata na vijiji wakifuatilia kikao cha kuhamasisha zoezi hilo.
45
Mkuu wa wilaya ya Kishapu, Mheshimiwa Nyabaganga Taraba (katikati) akiwa na Ofisa Mifugo na Maendeleo ya Mifugo wa wilaya, Dk. Aphonce Babyambagaki pamoja na Ofisa Mifugo anayeshughulikia minada.
6
Washiriki wa kikao hicho ambao ni maofisa mifugo kutoka kata mbalimbali na watendaji wa kata na vijiji wakifuatilia kikao.
………………………….
Na Robert Hokororo, Kishapu DC
Mkuu wa wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Mheshimiwa Nyabaganga Taraba amesema zoezi la utambuzi, usajili na ufuatiliaji wa ng’ombe kwa kutumia chapa litapunguza changamoto zinazowakabili wafugaji.
Alisema hayo jana wilayani hapa wakati akiongoza kikao cha maofisa mifugo pamoja na watendaji kata na vijiji kwa ajili ya kuhamasisha zoezi hilo linalotarajiwa kuanza Agosti 28 mwaka huu.
Mh. Taraba alibainisha kuwa Kishapu ni miongoni mwa wilaya ambazo baadhi ya wafugaji wake wanakabiliwa na matatizo yakiwemo wizi wa mifugo, migogoro na magonjwa hivyo zoezi hili litasaidia kuyapunguza.
Aidha aliwataka wataalamu wa mifugo na watendaji hao kufanya kazi kwa ushirikiano ili kufanikisha zoezi hilo ambalo linatarajiwa kufanyika vijiji vyote vya wilaya hiyo vyenye mifugo.
“Maofisa mifugo hakikisheni mnafanikisha zoezi hili siyo kusubiri ratiba hakuna atakayekusimamia na kazi lazima ziende ng’ombe anaugua wakati wowote na unapaswa kuwa tayari wakati wowote.
“Tunataka Kishapu tuwe mfano kwa kulifanikisha zoezi hili muhimu na nyie maofisa mifugo muwaelekeze watendaji wenu pale mnapokwamba muwasiliane na ofisi ya mkurugenzi watawasaidia,” alisisitiza.
Kwa upande wake Ofisa Mifugo na Maendeleo ya Mifugo wa halmashauri ya wilaya hiyo, Dk. Aphonce Babyambagaki aliwataka wataalamu hao kutumia taaluma zao kutoa elimu kwa wafugaji kuhusu umuhimu wa utambuzi na usajili wa ng’ombe.
Alisema hilo ni agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambalo linataka mifugo yote nchini kutambuliwa kwa kutumia chapa chini ya sheria ya utambuzi namba 12 sura namba 184.
Kaulimbiu yake ni sajili mifugo yako kwa uhakika wa soko na udhibiti wa wizi wa mifugo ambapo Dk. Babyambagaki alisema mifumo ya utambuzi iko miwili ikiwemo ya moto inayopigwa kwenye ng’ombe na hereni kwa wanyama wadogo.
Akifafanua zaidi alisema kutakuwa na alama ya kitaifa, wilaya na namba ya kijiji kwa kufuata mtiririko wa alfabeti ambayo huwekwa mguu wa kulia nyuma ya goti.
“Endapo mfugaji atapenda kuweka alama binafsi inapaswa kuwekwa upande wa mkono wa kulia chini ya kiwiko na iwe imesajiliwa kwa kuzingatia kanuni ya tisa ya usajili wa mifugo.

No comments