Header Ads

Responsive Ads Here

COAST UNION YA TANGA YAWANASA CHUJI,CASSILAS NA NTEBE KUANZA MAZOEZI JUMANNE UWANJA WA MKWAKWANI


IMG_0978

TIMU ya soka ya Coasta Union ya Jijini hapa, itaanza mazoezi kesho (Jumanne) kwenye uwanja wa Mkwakwani kujiwinda na Ligi Daraja la Kwanza (FDL), inayotarajiwa kuanza mwezi ujao huku ikitangaza nyota wake wapya iliyowasajili msimu huu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya timu hiyo Ahmed Hilal ‘Aurora’, alisema kazi ya usajili haina rahisi kutokana na kwamba kabla hawakuwa na fedha hivyo baada ya kurudisha umoja wameweza kusajili wachezaji wadhoefu watakaowasaidia kupanda daraja msimu huu.
Aurora aliwataja baadhi ya wachezaji wapya kuwa ni pamoja na mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, Simba na Yanga Athumani Idd ‘Chuji’, Hussein Sharrif ‘Cassilas’, Salvatory Ntebe kutoka Ndanda FC, Ramadhani Hassain kutoka Mbeya City, Maulid Rajab ‘Mau’ African Sports, Hilal Juma Mtibwa, Ramadhani Mussa Pamba, Ibrahim Ndanda, Baraka Jafar na Omary Salum kutoka African Lyion.
Aurora alitaja  wachezaji wengine ni pamoja na mfungaji bora wa Ndondo Cup iliyomalizika hivi karibuni Jijini Dar es salaam Rashid Roshi, Exavery Emanuel, Rahim Aziz Afrikan Lyon, Sagaf  Kabaki, Bakari Mtwiku, Bakari Nondo, Said Jeilani na Abubakari Kinanda ‘Mapara’ kutoka malindi ya Zanzibar.
Mwenyekiti huyo alisema usajili waliofanya ulizingatia mahitaji yaliyopo pamoja na tathimini waliyofanya baada ya kushuka daraja na kisha mwaka jana kushindwa kurejea Ligi kuu lakini pia umefanyika baada ya kuzika makundi yao na mpasuko.
Katibu wa klabu hiyo Nassor Kibabedi alisema mazoezi yataanza kesho kwenye uwanja wa Mkwakwani asubuhi kishajioni yatafanyika kwenye uwanja wa shule ya sekondari Galanos ambako mwalimu atakuwa Joseph Lazaro.

No comments