Header Ads

Responsive Ads Here

CHIRWA,KASEKE WASHINDA HUKUMU YAO MSUVA AKUTWA NA HATIA SASA TFF KUMPA BARUA


pic+yanga
Na.Alex Sonna
Hatimaye wachezaji watatu wa Yanga ambao walisimamishwa na bodi ya Ligi leo Kamati ya nidhamu ya TFF imewaachia huru  Obrey Chirwa na Deus Kaseke huku Simon Msuva akipewa onyo kwa njia ya maandishi baada ya kamati hiyo kubaini kuwa wachezaji hao hawakupaswa kupewa adhabu ya kusimamishwa.

Makamu mwenyekiti wa kamati ya nidhamu ya TFF,Peter Hella alisema kuwa kamati hiyo baada ya kupokea uteteza kwa wachezaji hao na kupata ushahidi wa picha ya mnato imebaini ni mchezaji pekee Simon Msuva ndiye aliyekutwa na makosa baada ya kumuangusha mwamuzi wa mechi husika kutokana na madai ya Yanga kunyimwa penalti.
Aidha amesema kuwa kamati hiyo itamuandikia barua ya onyo kali mchezaji Simon Msuva kwa kitendo chake ambacho alikifanya licha ya kuwa tayari alishaanza kutumikia adhabu ya kosa hilo ikiwemo kukosa kucheza baadhi ya mechi za Yanga kipindi ambacho timu hiyo ilishiriki michuano ya SportPesa.
Wachezaji hao kwa pamoja wakati wanaitumikia timu ya Yanga msimu uliopita walisimamishwa na kamati ya masaa 72 baada ya kuonekana wamemuangusha mwamuzi katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara uliowakutanisha Yanga na Mbao FC kwenye uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.
Mchezo huu Mbao FC walishinda kwa goli 1-0 lililofungwa na Habibu Haji baada ya makosa ya beki wa Yanga Vicent Andrew licha ya Simon Msuva kuhamia nchini Morocco huku Deus Kaseke akiwa amehamia katika timu ya Singida United ya Mkoani Singida

No comments