Header Ads

Responsive Ads Here

BARCELONA YAANZA VIZURI LA LIGA BILA SUAREZ NA NEYMAR YAITANDIKA REAL BETIS


Wakicheza bila ya mshambuliaji wao hatari Neymr amabye amehamia PSG pamoja na Luis Suarez aliye na majeruhi timu ya Barcelona imeanza vyema katika kusaka taji la Ligi Kuu ya Hispania kwa kupata ushindi wa magoli  2-0 katika mechi yake ya La Liga dhidi ya Real Betis.
Wakicheza kwa kujiamini licha ya kufungwa na mahasimu wao wakubwa Real Madrid katika mchezo wa Ngao ya Hisani walipata magoli yao kupitia  kwa Alin Tosco aliyejifunga dakika ya 36 huku beki Sergio Roberto akipingilia msumari wa pili dakika ya 39.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko hata hivyo mabadiliko hayo hayakuweza kuwasaidia Real Betis hadi dakika 90 Barcelona wameibuka na ushindi wa jumla ya magoli 2-0 na pointi tatu muhimu.
Katika Uwanja wa Camp Nou, kulikuwa na ulinzi wa ziada kutokana na shambulio la kigaidi lililotokea siku tatu zilizopita na kusababisha vifo vya watu 14.

No comments