Header Ads

Responsive Ads Here

BANTU-AJALI NYINGI ZASABABISHWA NA KU-OVERTAKE PASIPO TAHADHARI /MADEREVA WAWE MAKINI


IMG_20170823_115922
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
AJALI nyingi hutokea kutokana na matumizi ya kupita gari ama magari mengine pasipo kuchukua tahadhari (overtake)ambapo imeelezwa ni asilimia 62 ya ajali hizo.

Kutokana na chanzo hicho ,madereva wanatakiwa kuwa makini na kuchukua tahadhari ili kuepuka ajali zembe.
Akizungumza katika mafunzo ya siku tatu ya uandishi wa namna ya kuandika habari za usalama barabarani  ,yaliyoandaliwa na Tamwa yanayofanyika wilayani Kibaha, mkufunzi wa masuala ya barabarani katika semina hiyo ,Henry Bantu ,alisema ajali nyingi husababishwa na hatari zinazotegemewa .
Alieleza ,moja ya hatari zinazotegemewa ni sanjali na Ku -overtake bila kuwa makini hali inayosababisha ajali na kupelekea vifo na majeruhi .
Bantu alisema ,hakuna sheria inayosema lazima kupita gari na magari mengine .
“Hakuna sababu ya kupita gari lililopo mbele yako ,labda kuwe hakuna hatari mbele yako ,sasa unakuta madereva wengi hufanya maamuzi hayo kuwahi shughuli zao bila kujali kama kutatokea ajali” alifafanua .
Alieleza kwamba ,sheria nyingi zilizokuwepo miaka ya nyuma sasa hazifuatwi .
Aidha Bantu alisema ,sheria ya mwaka 1972 imeshabadilika kwa kukiukwa kwasababu ya wakati unavyozidi kwenda na magari kuongezeka .
Alisema ,udereva ni kujihami na ndio umahiri ili kuzuia ajali barabarani .
Bantu aliwataka madereva wafuate sheria na kujali maisha ya abiria wanaowabeba ,na kuacha kwenda mwendo kasi ,kutoendesha wakiwa na uchovu,kutumia vileo ,kutumia simu wakati wa kuendesha 
“Ukiona dereva unaenda mahakamani jua umeharibu  kwenye ukiukwaji sheria .” alisema Bantu .
Aliwataka waandishi wa habari watumie kalamu na nyenzo za tasnia hiyo kuhubiri kwa madereva waachane na udereva wa kukiuka sheria za usalama barabarani.
Nae mratibu wa mradi wa usalama barabarani kutoka Tamwa ,Gladys Munuo ,alisema mafunzo hayo yana lengo la kuwapa uwezo wanahabari waweze kuandika masuala ya usalama barabarani kwa ufanisi na kufanya uchunguzi ili kuelimisha jamii na madereva .
Alisema kuna kila sababu ya kufanyiwa maboresho na marekebisho  sheria ya mwaka 1973 ambayo ina baadhi ya maeneo yenye mapungufu .
Gladys alitoa mfano sheria hiyo inamruhusu dereva kuwa na kiwango cha kilevi cha asilimia 0.08 wakati kimataifa ni 0.05 kiwango ambacho ni kikubwa .
Dereva kuruhusiwa na biria wake wa mbele kufunga mkanda bila kujali abiria wa nyuma na sheria hiyo inaeleza dereva wa pikipiki ndie anawesa kuvaa kofia ngumu na sio mteja wake .
Gladys alieleza kuwa , wanasheria na wadau mbalimbali sanjali na Tamwa ,wanaona kuna haja kufanyiwa maboresho kwa sheria hiyo ya 1973 .
Akizungumzia mradi wa masuala ya usalama barabarani alisema hayo ni mafunzo ya tano tangu waanze kutoa elimu na wanatarajia kufikia waandishi wa habari 80.
Kwa upande wake kamanda wa Polisi Mkoani Pwani ,kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Jonathan Shanna alisema wamejiwekea mikakati ya kudhibiti ajali mkoani hapo.
Alitoa ushauri kwa mamlaka kama wizara ya ujenzi na wakala wa barabara TANROADS na halmashauri za miji na wilaya katika uwekaji wa alama na michoro ya barabarani .
Kamanda Shanna alisema, watasimamia kwa karibu mfumo wanutoaji leseni za udereva ili kila atakayepata leseni hiyo awe amepitia chuo cha udereva na kufaulu .
Alibainisha wataomarisha utoaji wa elimu ya usalama barabarani kwa shule za msingi ,sekondari na vyuo .
Kamanda huyo ,alitoa rai kwa wamiliki wa magari ya abiria na binafsi  kufanya matengenezo ya magari yao pindi yanapokuwa na hitilafu ili kuepukana na ajali ambazo hugharimu maisha ya watu.
“Uchunguzi uliofanyika umebaini madereva wa pikipiki maarufu bodaboda wanajali na kuthamini kukimbilia pesa zaidi kuliko kujali maisha ya watu wanaowapakia.” alisema kamanda Shanna.
Aliwaasa madereva kijumla wabadilike ,wafuate sheria iliopo ili kuepuka  kugharimu maisha ya watu na wengine kubakia na ulemavu wa viungo.
Katika hatua nyingine ,afisa wa masuala ya usalama barabarani kutoka shirika la afya duniani (WHO),Mary Kessi ,alisema tafiti zinaonyesha watu mil.1.2 hufariki dunia kutokana na ajali kwa mwaka.
Kwa Tanzania inadaiwa watu 16,000 hufa kutokana na ajali kwa mwaka ambapo kati yao wanaopoteza maisha zaidi ni vijana wenye umri 15-29.
Mary alielezea,kulingana na takwimu zilizokusanywa kutoka nchi 180, inaonesha idadi ya vifo kila mwaka kutokana na ajali za barabarabi inapungua. 

No comments