Header Ads

Responsive Ads Here

BANDA AINUSURU BAROKA SWALLOWS DHIDI YA ORLANDO PIRATES MECHI YA LIGI KUU AFRIKA KUSINI


BANDA
Abdi Banda amefunga bao lake la kwanza katika Ligi Kuu Afrika Kusini (PSL) na kuikoa timu yake ya Baroka Swallows kuwakomalia vigogo, Orlando Pirates kwa sare ya bao 1-1.
 
Baroka FC waliokuwa nyumbani, walikubali kuruhusu bao katika dakika ya 41 baada ya Thabo Qalinge kuinfungia Orlando bao la kwanza.
Vigogo hao wanaofundishwa na Kocha Mserbia, Sredojevic Milutin walikwenda mapumziko wakiwa wanaongoza kwa bao 1-0, ikionekana kama wana nafasi ya kuongeza bao la pili katika kipindi cha pili.
Lakini Banda aliyekuwa anaongoza safu ya ulinzi alikuwa imara na dakika ya 73 alifunga bao safi na kuisawazishia timu yake.

No comments