Header Ads

Responsive Ads Here

ASKOFU DKT MDEGELLA AANZA KUNUSURU CHUO CHA TUMAINI MAKUMIRA TAWI LA MBEYA KUPIGWA MNADA

Askofu  Dkt.  Mdegella  akizungumza na  wanahabari

Na  MatukiodaimaBlog

KATIKA  harakati  za  kukinusuru  Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira  tawi la  Mbeya kisipigwe  mnada  na benki  ya biashara ya  Afrika (CBA) Askofu  Mstaafu  wa Kanisa la  Kiinjili la  Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya  Iringa ambae  pia ni Mwenyekiti wa bodi ya chuo hicho,   Dkt  Owdenburg Moses Mdegela amesema  ameamua  kujilipua kunusuru  chuo  hicho  kwa  kuanza  kutembeza  bakuri kwa  waumini  wote wa KKKT  nchini  wakiwemo viongozi  na  wanasiasa  ambao ni  walutheri kama  mke wa Rais wa awamu ya  tatu mama Anna Mkapa   na  wengineDkt  Mdegella  amesema  amechukua  hatua  hiyo  ya  kujilipua  baada ya  kuona  dalili   ya  chuo  hicho  kupigwa  mnada akizungumza  na  wanahabari  juu ya hatua  hiyo  aliyochukua Dkt. Mdegela a alisema chuo hicho ambacho ni sehemu ya kanisa hilo kipo katika hatari ya kuzama kwa kushitakiwa na kuuziwa  mali zake, na kuitia aibu KKKT kama uvumilivu wa benki hiyo  utafika mwisho kwa kushindwa kulipa deni hilo.

 Alisema ameamua kujilipua na kuomba
 msaada huo kupitia vyombo vya habari baada ya kuona jitihada
 na mikutano mingi ya kulipa deni na malimbikizo yake ya riba
 kwa kupitia taratibu za kawaida za kanisa yakipata vikwazo
 kila wanapokutana kujadili.

 Alisema Desemba, 2013 chuo hicho
 kilikopa kutoka katika benki hiyo zaidi ya Sh Bilioni 1.6
 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la utawala na madarasa ya chuo;
mkopo ambao sehemu yake haukutumika kwa kazi iliyokusudiwa.

Bila kutaja majina ya wahusika wa
 matumizi mabaya ya fedha za mkopo huo, Dk Mdegela alisema
 baadhi ya wajumbe wa bodi na viongozi wa chuo hicho
 wanapaswa kubeba lawama na kuchukuliwa hatua za kisheria
 kutokana na ubadhirifu uliofanywa.

 “Tumefanya ukaguzi wa hesabu za mkopo
 huo mara mbili. KKKT ilifanya ukaguzi wake lakini pia
kulikuwa na mkaguzi wa nje. Kwa pamoja wamebaini kuwepo kwa  ubadhirifu mkubwa, rushwa na ufisadi” alisema.

 Alisema ukaguzi wa awali unaonesha
 asilimia 45 ya mkopo huo ndiyo iliyotumika kwa kazi
 iliyokusudiwa huku asilimia 55 iliyobaki ikitumika kwa
 malengo tofauti na ujenzi uliokusudiwa.

 “Suala hili limeshakabidhiwa Polisi
 na kwa wanasheria ili hatua za kisheria kwa wahusika
 zichukuliwe. Na kwa taarifa ni kwamba wahusika wanaotuhumiwa  kwa ubadhirifu huo wamekwisha simamishwa kazi,” alisema bila kuwataja wahusika hao.
 Dk Mdegela ambaye pia ni mwenyekiti wa
 timu ya maaskofu watatu wa kunusuru chuo hicho (Dk Mdegela,
Dk. Alex Malasula na Dk Abednego Mshahara)  alisema kwa
makubaliano ya kulimaliza suala hilo kiungwana, benki hiyo
 imewataka kulipa Sh Milioni 275 ifikapo mwishoni mwa mwezi
 huu na kwamba marejesho ya deni hilo yataendelea kufanywa
 kila mwezi.

 “Mahali lilipofika suala hili sio
 mahali pa  kunyamaza, tunataka kila mlutheri na sharika
 zake zote nchini zijue kinachoendelea na wachangie kunusuru
 chuo hicho ili kuliondolea kanisa aibu,” alisema.

 Alisema ili kufikia makusanyo hayo
 kutakuwa na makundi manne, la kwanza litajumuisha watu
 watakaombwa kuchangia Sh 100,000 na kuendelea, la pili
 watachangia kati ya Sh 50,000 na Sh 100,000, la tatu kati ya
 Sh 20,000 na Sh 50,000 na la nne kiasi chochote chini ya Sh
 20,000.

Pamoja na mapendekezo hayo alisema,
 watu wataruhusiwa kuchanga zaidi ya kiwango
 kinachopendekezwa katika makundi yao kwa kadri
 watakavyoguswa na jambo hilo alilosema ni tatizo kwa
 kanisa.

 “Lakini pia nitalazimika kukutana na
 walutheri maarufu ambao ni waajiriwa katika taasisi
mbalimbali, wafanyabishara na wanasiasa na wadau wengine wa
 KKKT nchini,” alisema na kuwataja baadhi yao kuwa ni
 pamoja na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi na  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk Charles Kimei.

Pamoja na kupitisha kapu hilo, alisema
 wanaendelea kuandaa njia nyingine zitakazosaidia kufikia
lengo la makusanyo na marejesho ya deni hilo hadi
 litakapokwisha.

Dk Mdegella aliwataka wadau hao
kuchangia chuo hicho kupitia akaunti maalumu No 108433100028
iliyofunguliwa katika benki hiyo ya CBA kwa ajili ya
 kukusanya na kulipa deni hilo.

 Alisema yote hayo anayafanya kwa niaba
 ya Mkuu wa Kanisa, Askofu Dk Frederick Shoo na kwa niaba ya
 askofu wa dayosisi ya Iringa, bodi ya wadhamini ya chuo,
baraza la uongozi na maaskofu wenzake na wajumbe waliopewa
 kazi ya kunusuru chuo hicho.

Kwa yoyote anayehitaji ufafanuzi
 zaidi anaweza kuwasiliana jinsi ya kukisaidia chuo hicho
kupitia simu namba
 0754313173,” alisema.

No comments