Header Ads

Responsive Ads Here

AKINAMAMA WAJAWAZITO KUPATA HUDUMA YA UPASUAJI KITUO CHA AFYA CHALINZE-DR HANGAI


Operations 1
Na Mwamvua Mwinyi, Chalinze
KITUO cha afya cha Chalinze, Bagamoyo mkoa wa Pwani kimeanza kutoa huduma ya upasuaji kwa akinamama wajawazito wenye mahitaji hayo.
 
Utekelezaji huo umebainika baada ya mbunge wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Kikwete kutaka kupatiwa uhakika wa jambo hilo,katika baraza la madiwani.
Ridhiwani alisema anasikia sikia kwa baadhi ya wananchi kuhusiana na jambo hilo hivyo ni vyema ikatangazwa rasmi.
Alieleza hizo ni taarifa njema kwa wananchi wa Chalinze hasa wanawake ambao walikuwa wakipata kero ya kwenda kupatiwa huduma hiyo nje ya Chalinze .
Kwa upande wake mganga mkuu wa halmashauri ya Chalinze dr. Rahim Hangai ,alisema wameanza kutoa huduma hiyo mwezi uliopita na itakuwa kwa wajawazito pekee kutokana na huduma kupatikana jengo la uzazi.
Alibainisha tayari akina mama kumi wajawazito wameshapatiwa huduma ya upasuaji kituoni hapo.
Dr .Hangai alisema hakuna kifo wala madhara yaliyojitokeza hadi sasa kwani wote waliohudumiwa wapo salama kiafya.
“Kituo hicho kimeshaanza kutoa huduma ya upasuaji ambayo ni muhimu,akina mama wajawazito ambao wamebainika hawana uwezo wa kusukuma mtoto walifanyiwa upasuaji na walikuwa na hali nzuri,” alisema Dr. Hangai .
Nae mwenyekiti wa halmashauri hiyo Saidi Zikatimu alisema awali wananchi wa Chalinze walikuwa wakihangaika kwa kukosa huduma ya karibu ya upasuaji.
Alielezea kuwa ,kwasasa wataepukana na adha ya safari ndefu kufuata huduma hiyo hospital ya rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi,hospital ya wilaya Bagamoyo na hospital ya taifa Muhimbili iliyopo jijini Dar es salaam .
Zikatimu alisema,pia mafuta yaliyokuwa yakitumika kusafirisha wagonjwa kwenda maeneo hayo,yatatumika kwenye shughuli nyingine.
Hata hivyo ,alisema wanatarajia kujenga uzio kutoka chumba cha upasuaji kwenda wodini ili mgonjwa asiwe kuonekana na watu wengine mara atokapo kufanyiwa huduma,” alisema Zikatimu.

No comments