Header Ads

Responsive Ads Here

AJIBU AING’ARISHA YANGA DHIDI YA CHIPUKIZI MCHEZO WA KIRAFIKI UWANJA WA GOMBANI PEMBA


20914577_478312132548570_1509878309435400449_n
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara klabu ya Yanga imeendelea na mazoezi katika uwanja wa Gombani Visiwani Pemba ambapo imeweka kambi kwa ajili ya mechi ya Ngao ya Hisani dhidi ya Mahasimu wao wa Jadi Simba mchezo utakaopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Agosti 23 ya Jumatano.

Wakiwa visiwani humo wamecheza mchezo mmoja wa kirafiki dhidi ya timu ya Chipukizi na Yanga kupata ushindi wa bao 1-0 likifungwa na mshambuliaji wao mpya Ibrahim Ajibu kipindi cha kwanza.
Huu ni mwendelezo wa Ajibu kufunga kwani kabla ya kwenda Pemba walipita visiwani Ugunja na kucheza na Mlandege na Yanga walipata ushindi wa jumla ya mabao 2-0 yakifungwa na Ibrahim Ajibu na Emmanuel Martin.
Kuendelea kufunga kwa Ajibu kuna leta imani kwa mashabiki wa timu hiyo kuelekea kwenye mechi ya Dar es salaam Derby yenye upinzani mkubwa barani Afrika

No comments