Header Ads

Responsive Ads Here

ZANZIBAR YAFUTWA UANACHAMA WA CAF


Ahmad-700x367
Rais wa soka barani Afrka (CAF ) Ahmad Ahmad.

Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limefanya maamuzi ya kuwavua uanachama chama cha soka cha Zanzibar ikiwa ni miezi minne toka  kipewe uanachama na CAF kutoka kwa Rais aliyepita Issa Hayatou.
 
Rais wa soka barani Afrka (CAF ) Ahmad Ahmad amesema Zanzibar walipewa uanachama kimakosa na kama sheria zingepitiwa vizuri wasingepewa uanachama.
“Walipewa uanachama bila kupitia vizuri kanuni ambazo ziko wazi na zinaeleza kila kitu, kama kanuni na sheria zingepitiwa kiufasaha wasingepewa uanachama”
Sababu kubwa ambayo CAF wameivua uanachama Zanzibar ni kutokana na kisiwa hicho kuwa ndani ya Tanzania ambao nao ni wanachama wa CAF.
“Jina la nchi linatokana na jina linaloandikwa katika umoja wa mataifa UN na Zanzibar katika umoja huo inafahamika ipo ndani ya nchi iitwayo Tanzania ambao ni wanachama wa CAF” alisema Ahmad.
Hilo ni pigo kubwa kwa Wazanzibar kwani wakati huu walikuwa wakipambana kupata uanachama wa FIFA ambao wameukosa na wa CAF nao pia wamekosa.
Kwa maana hiyo ndoto ya kisiwa cha Zanzibar kushiriki michuano ya CAF kama mwanachama zimekufa rasmi na sasa watakuwa wakishiriki michuano hiyo kama Tanzania (Zanzibar na Tanzania bara).

No comments