Header Ads

Responsive Ads Here

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII KUPITIA TAWA YAPOKEA MISAADA YA KUPAMBANA NA UJANGILI


TAASISI YA KIMATAIFA YA KIJAMII YA UHIFADHI WA WANYAMAPORI YA WCS IMETOA MSAADA WA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 940 AMBAZO ZIMETUMIKA KUJENGA OFISI, KUNUNUA VITENDEA KAZI YAKIWEMO MAGARI NA KUGHAMARAMIA MAFUNZO KWA ASKARI WA WANYAMAPORI WA MAPORI YA AKIBA YA LUKWATI- PITI ILI KUKABILIANA NA UJANGILI NA UWINDAJI HARAMU AMBAO UMESABABISHA VIFO VYA TEMBO WAPATAO 23 TANGU MWAKA 2013 MPAKA SASA.

MENEJA WA MAPORI HAYO YA AKIBA YA LUKWATI/ PITI ALPHONCE AMBROCE MUNG’ONG’O AMESEMA MAPORI HAYO MAWILI YENYE UKUBWA WA ZAIDI YA KILOMITA ZA MRABA 6,119 YALIYOKO LUPA TINGATINGA MKOANI SONGWE YANATUMIKA KWA UWINDAJI WA KITALII WA WANYAMAPORI AMBAYO KATIKA KIPINDI CHA MIAKA MITANO ILIYOPITA YAMEIINGIZIA SERIKALI MAPATO YA ZAIDI YA DOLA ZA KIMAREKANI MILIONI 1.3 SAWA NA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI MBILI NA MILIONI MIA NANE NA AMEWAONYA WATU WANAOJIHUSISHA NA UJANGILI KUWA SASA WATAFUTE KAZI NYINGINE:

AKIONGEA KATIKA HAFLA YA KUKABIDHI MIRADI HIYO IKIWEMO JENGO LA KISASA, MAGARI NA VIFAA VYA DORIA KWA SERIKALI YA TANZANIA, MKURUGENZI WA TAASISI YA KIJAMII YA KIMATAIFA YA UHIFADHI WA WANYAMAPORI IITWAYO WORLD CONCERVATION SOCIETY, AARON NICHOLAUS AMESEMA WCS INAJIVUNIA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI YA TANZANIA KATIKA KUIMARISHA UHIFADHI NA AMEZUNGUMZIA UMUHIMU WA MAPITO YA WANYAMAPORI AMBAYO YAMEATHIRIWA NA SHUGHULI ZA BINADAMU LICHA YA UMUHIMU WAKE KWA UHIFADHI AMBAPO KATIBU MKUU WIZARA YA MALIASILI NA UTALII MEJA JENERALI GAUDANCE MILANZI AMESEMA MSIMAMO WA SERIKALI YA TANZANIA KATIKA UHIFADHI UKO WAZI KWANI MALIASILI HIZO ZINA UMUHIMU KWA MAENDELEO YA TAIFA:
MKURUGENZI WA SHIRIKA LA WCS (KULIA) AKIKABIDHI MAGARI 3 KWA KATIBU MKUU WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII MEJ.GEN.GAUDENCE MILANZI (MWENYE KOTI) KWA AJILI YA KUKABILIANA NA UJANGILI KATIKA PORI LA AKIBA LUKWATI/PTI

KAIMU MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA WANYAMAPORI TANZANIA TAWA, MARTIN LOIBOOKI AMESEMA TAWA INATAMBUA WAJIBU WAKE NA MALENGO YA KUANZISHWA KWA MAMLAKA HIYO YA KUSAIDIA KUCHOCHEA MAENDELEO YA JAMII NA KUKUZA UCHUMI WA NCHI KUPITIA SEKTA YA WANYAMAPORI NA AMEISHUKURU WCS KWA KUWA MFADHILI WA KWANZA KUFADHILI SHUGHULI ZA UHIFADHI KATIKA MAPORI YA LUKWATI- PITI


BW.MARTIN LOIBOOKI(KAIMU MKURUGENZI MKUU-TAWA) AKISOMA RISALA MBELE YA KATIBU MKUU TAARIFA KUHUSU MAPORI YA LUKWATI NA PITI NA SAADA UTAKAVYOTUMIKA

No comments