Header Ads

Responsive Ads Here

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsaia,Wazee na Watoto atembelea hospitali ya Wilaya ya Chato


soz1
Waziri  wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akikagua risiti  ya mmoja wa mama aliyefika kwenye hospitali ya Wilaya ya Chato aliyekuwa amemleta mtoto wake kupata matibabu.Mhe.Waziri alikua akijiridhisha kama mama huyo amelipishwa fedha katika  matibabu ya mtoto kwakuwa matibabu kwa mtoto chini ya miaka mitato huduma hutolewa bila malipo

soz2
Waziri Ummy akikagua duka la dawa lililopo kwenye hospitali hiyo (Duka la MSD) ambalo linasaidia upatikanaji wa dawa  katika hospitali hiyo pamoja na vituo vya afya pamoja na zahanati za jirani.Kulia mwisho ni Mbunge wa Jimbo la Chato na naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini Dkt.Medard Kalemani
soz3
Waziri wa Afya akitoka kutembelea Wodi ya Wazazi iliyopo kwenye Hospitali hiyo,kushoto ni Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt. Athanasi Ngambakub na katikati ni Naibu Waziri wa Nishati na madini Dkt.Medard Kalemani
soz4
Waziri Ummy wakijadiliana jambo kwenye jengo jipya linalojengwa la upasuaji,ambapo Waziri ameagiza jengo hilo likikamilika wawape kipaumbele akina mama wajawazito ili kuweza kuokoa vifo vitokanavyo na uzazi
soz5
Katika wodi waliyolazwa watoto Waziri Ummy akimsalimia mmoja wa mtoto aliyelazwa hospitalini hapo
soz6
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akimsisitiza jambo Waziri wa Afya wakati wa kuongea na watumishi wa hospitali hiyo,kushoto ni Mkuu wa Wilaya Mhe.Shabani Ntalambe
soz7
Dkt.Kalemani akizungumza na watumishi wa hospitali hiyo(hawapo pichani) mara baada ya kutembelea hospitali hiyo
soz8
Meneja wa Kanda ya Mwanza wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD) Victory Sungusia akijibu swali toka kwa Waziri Ummy wakati wa kuongea na watumishi wa hospitali ya Wilaya ya Chato
soz9
Baadhi ya watumishi wa hospitali hiyo wakimsikiliza Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto(hayupo pichani)
soz10
Picha ya pamoja ya Mawaziri,Viongozi wa Mkoa na Wilaya pamoja na baadhi ya watumishi wa hospitali hiyo mara baada ya kumaliza ziara (Picha zote na Wizara ya Afya)

No comments