Header Ads

Responsive Ads Here

WAZIRI MKUU AWAASA WATUMISHI WANAOFANYAKAZI VIWANDANI


PMO_6640
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa umma wa wilaya ya Rungwe Julai 30, 2017. Kulia ni Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson na kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

PMO_6671
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa kiwanda cha gesi cha TOL Gasese Limited kilichopo katika kijiji cha  Ikama wilayani Rungwe Baada ya kuwasili kiwandani hapo Julai 30, 2017 Kushoto ni Naiobu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_6673
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana viongozi wa kiwanda cha chai cha Katumba wilayani Rung wakati alipowasili kiwandani hapo kukagua shuguli za kiwanda hicho Julai  30, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_6687
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akitembelea kiwanda cha chai cha Katumba wilayani Rungwe Julai 30, 2017. Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Mbeya  Amos Makalla na kushoto ni Meneja Uzalishaji wa kiwanda hicho, Ramadhani Kampasili. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_6735
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akitazama  chai iliyosindikwa na kufungashwa tayari kwa kuuzwa wakati alipotembelea kwianda cha chai cha Katumba wilayani Rungwe Julai 30, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri )
PMO_6770
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Rungwe baada ya kutembelea kiwanda cha Chai cha Katumba Julai 30, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_6809
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akipata maelezokutoka kwa  Mkutugenzi wa Ufundi, Bw. McJohn Mbiri  (kulia Kwake)  kuhusu mitambo ya kuzaisha gesi ya hewa ya ukaa wakati alipotembelea kiwanda cha TOL Limited  kilichopo katika kijiji cha Ikama wilayani Rungwe Julai 30, 2017. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_6847
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wazee wa Busokelo baada ya kuwasili kwenye uwanja wa michezo wa Kandete katika jimbo la Busokelo kuhutubia mkutano wa hadhara Julai 30, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_6883
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifuhia ngoma ya asili baada ya kuwasili kwenye uwanja wa michezo wa Kandete  katika jimbo la  Busokelo mkoani Mbeya kuhutubia mkutano wa hadhara Julai 30, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_6238
Baadhi ya watumishi wa umma wa wilaya ya Rungwe wakati alipozungumza nao leo Julai 30, 2017.
…………………………………………………………………..
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewasihi Watanzania wanaofanya kazi katika viwanda mbalimbali nchini kufanya kazi kwa bidii na kuwa waaminifu.
 Amesema Tanzania imedhamiria kukuza uchumi wake kupitia sekta ya viwanda hivyo ni vema watakaopata fursa ya ajira katika viwanda hivyo kuwa waadilifu.
 Ameyasema hayo leo (Jumapili, Julai 30, 2017) wakati akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha gesi cha Ikama kilichoko wilayani Rungwe.
 Waziri Mkuu amesema wakati Serikali ikiendelea kuwakaribisha wawekezaji nchini, wananchi walioajiriwa kwenye maeneo hayo wawe waaminifu.
 “Mnatakiwa muwe waaminifu, msibebe kitu chochote ndani ya kiwanda bila ya ridhaa ya wamiliki kwa kuwa mtaonyesha taswira mbaya kwa wawekezaji.”
 Amesema uaminifu wao ndio utawezesha Watanzania wengi kupata ajira kwenye viwanda hivyo ambavyo vimejengwa  katika maeneo yao.
 Awali, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kiwanda hicho kinachomilikiwa na kampuni ya TOL Gases, Mhandisi  Harold Temu alisema kiwanda kinauwezo wa kuzalisha tani 46 kwa siku.
 Alisema gesi inayozalishwa kiwandani hapo ni ya Carbon Dioxide ambayo inauzwa nchini na nchi jirani za Zambia, Malawi, Zimbabwe na Congo.
 Mhandisi Temu alisema wateja wakubwa wa gesi hiyo ni viwanda vya kutengenezea soda, bia na pia hutumika katika kuhifadhia chakula na kwenye vifaa vya kuzimia moto.
 Mapema Waziri Mkuu alitembelea kiwanda cha kuchakata majani ya chai cha Katumba, ambapo alisema Serikali inaimarisha Ushirika wa zao hili ili wakulima waweze kupata tija.

No comments