Header Ads

Responsive Ads Here

WANANCHI WA KARAGWE WAIPONGEZA SERIKALI


j (1)
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, Selemani Jafo akiwa na Mkuu wa wilaya ya Karagwe Godfrey Mheruka akifanya ukaguzi wa ujenzi wa wodi ya wazazi katika Kituo cha Afya Kayanga.

j (2)
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na Mbunge wa Karagwe Innocent Bashungwa , Mkuu wa wilaya ya Karagwe Godfrey Mheruka pamoja na watumishi wa Idara ya Afya.
j (3)
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akikabidhiwa zawadi ya mbuzi na wananchi wa kijiji cha Ihembe baada ya ufunguzi wa Ofisi mpya ya walimu.
j (4)
Wanafunzi wa Shule ya msingi Ihembe wakicheza ngoma kwa furaha katikati ni Mkurugenzi wa Miundombinu kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi Henry Katabwa.
j (5)
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi akiwapongeza wadau walioshirikiana na Rwakilomba katika ujenzi wa Ofisi za walimu pamoja na darasa shuleni Ihembe.
j (6)
j (7)
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akifurahi jambo na viongozi na watumishi wa wilaya ya Karagwe baada ya kukagua ujenzi wa wodi ya wazazi.
………………………………………………………………………
Wananchi wa wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera wameipongeza serikali kwa kazi kubwa inayofanya ya kuwaletea maendeleo wananchi wake.
 Pongezi hizo wamezitoa leo katika ziara ya kikazi ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo alipotembelea wilayani humo kukagua miradi ya maendeleo
 Katika ziara yake, Naibu Waziri Jafo amefanikiwa kukagua ujenzi wa wodi ya wazazi na jengo la kuhifadhia maiti katika kituo cha Afya kayanga, ujenzi wa kituo kipya cha afya Nyakayanja, na alizindua Ofisi za walimu na darasa   katika shule ya msingi Ihembe. 
 Wananchi hao wamesema wanaishukuru serikali na kuipongeza kwa jitihada ambazo wamezichukua za kutatua changamoto zinazowakabili na kuwaletea maendeleo.
 Akizungumza na wananchi hao, Jafo amewaeleza wananchi mpango wa serikali wa kukiboresha kituo cha afya kayanga kwa kujenga chumba cha upasuaji na majengo mengine muhimu ndani ya mwaka huu ili kituo hicho cha afya kiweze kutoa huduma bora ya upasuaji kwa lengo la kupunguza vifo vya mama wajawazito.
 Akifungua Ofisi ya walimu na darasa katika shule ya msingi Ihembe, Naibu Waziri Jafo amempongeza Filbert Rwakilomba kwa kushirikiana na wadau wake kutoka Ofisi ya Tamisemi kufanikisha ujenzi huo na amewataka watanzania wengine kuiga mfano huo.

No comments