Header Ads

Responsive Ads Here

WANANCHI GEITA WATAKIWA KUJENGA DESTURI YA KUFANYA MAZOEZI MARA KWA MARA


Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl,Herman Kapufi akiongoza wananchi kufanya mazoezi kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Geita.
Mazoezi yakiendelea kwa wananchi

Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi akiendelea kuelekeza mazoezi mbali mbali ya viungo.


Mkurugenzi wa Mazoea GYM ,Bi Mazoea Salum akielezea juu ya ushiriki wa wanawake kutokupenda kujitokeza kwenye mazoezi ya viungo.

Mwalimu wa mazoezi ambaye anatokea mazoea Gym  Valence Ibrahim akizungumzia juu ya kuendelea wananchi kujitokeza kufanya mazoezi kila siku ya jumamosi.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita.Mhandisi Modest Aporinaly akisisitiza wananchi kujenga Desturi ya kufanya Mazoezi.

Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akielezea faida ambazo zinaweza kupatikana kutokana na kufanya mazoezi na kwamba hataakikisha kila mwananchi ambaye yupo kwenye wilaya ambayo anaiongoza anajenga Desturi ya kufanya mazoezi ya viungo.

Mkuu wa Wilaya akipata picha ya pamoja na baadhi ya wadau ambao wamejitokeza kwenye mazoezi.
(PICHA NA JOEL MADUKA WA MADUKA ONLINE)
 
Wananchi Wilayani na Mkoani Geita wametakiwa kujenga desturi ya kupenda kufanya mazoezi ya viungo mara kwa mara hili kuepukana na maradhi ambayo yanaweza kutokana kwasababu ya kutokufanya mazoezi.
Rai Hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Geita ,Mwl Herman Kapufi wakati wa ufunguzi wa Kapufi Bonanza ambapo lengo ni kuwajengea wananchi kwenye Wilaya anayoiongoza kujenga tabia ya kufanya mazoezi.
Kapufi,amesema kuwa hipo sababu ya wananchi kwenye wilaya hiyo kufanya mazoezi kwani yanaufanya mwili kuwa imara na kukabiliana na magonjwa kama ya presha.
Pia amewataka wakazi wa Wilaya hiyo kujitokeza jumamosi ya Wiki ijayo kwenye mazoezi ambayo yanatarajia kuanzia kwenye ofisi za Wilaya na kuelekea kwenye viwanja vya shule ya Sekondari Kalangalala.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mazoea GYM ,Bi Mazoea Salum amesikitishwa na idadi ndogo ya wanawake pamoja na mabinti kwenye mazoezi na kuwataka kujitokeza kwa wingi zaidi kila siku ya jumamosi hili na wao pia waweze kuhimalisha afya zao.

No comments