Header Ads

Responsive Ads Here

WABUNGE NANE WA CHAMA CHA CUF WAPOTEZA UBUNGE


index
BUNGE LA TANZANIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kufuatia barua aliyopokea Spika wa Bunge Mhe. Job Yustino Ndugai kutoka kwa Mwenyekiti Prof. Ibrahim Haruna Lipumba  na Kaimu Katibu Mkuu Mhe. Magdalena Hamisi Sakaya (Mb) wa Chama cha Wananchi (CUF), Mheshimiwa Spika angependa kuwaarifu Watanzania wote kwamba amejiridhisha kuwa Wabunge hao wamefukuzwa Uanachama kulingana na taratibu za Chama hicho na hivyo wamekosa sifa za kuendelea  na Ubunge.  Wabunge hao ni: –
 
  1. Mhe. Severina Silvanus Mwijage, (MB);
  2. Mhe. Saumu Heri Sakala, (MB);
  3. Mhe. Salma Mohamed Mwassa, (MB);
  4. Mhe. Riziki  Shahari Mngwali, (MB);
  5. Mhe. Raisa Abdallah Mussa, (MB);
  6. Mhe. Miza Bakari Haji, (MB);
  7. Mhe. Hadija Salum Ally Al-Qassmy, (MB); na
  8. Mhe. Halima Ali Mohamed, (MB).
Hivyo, kwa mamlaka aliyonayo kwa kuzingatia kifungu cha 67(1)(b) cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 kikisomwa pamoja na kifungu 37(3) cha Sheria ya Uchaguzi Sura 343 kama ilivyojadidiwa Mwaka 2015, Mheshimiwa Spika ametangaza nafasi hizo kuwa wazi na pia kumuandikia  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ili aendelee na hatua zinazostahili  kujaza  nafasi hizo kwa Mujibu wa  Sheria na Taratibu zilizopo.
Imetolewa na:
        Ofisi ya Spika,
  1. L. P. 941,
        DODOMA.
        26 Julai, 2017

No comments