Header Ads

Responsive Ads Here

WAASTAFU WA JESHI LA MAGEREZA WAAGWA RASMI JIJINI DAR


PIX 1
Naibu Kamishna Mstaafu wa Magereza, Edith Malya akiwa kwenye gari maalum pamoja na Wastaafu wengine wa Jeshi la Magereza wakipita katikati ya Gwaride likiwa katika umbo la OMEGA ikiwa ni ishara ya kuwaaga rasmi baada ya kustaafu utumishi wao Jeshini. Hafla hiyo imefanyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam Julai 21, 2017.

PIX 3
Naibu Kamishna Mstaafu wa Magereza, Edith Malya akiwa kwenye gari maalum pamoja na Wastaafu wengine wa Jeshi la Magereza wakiwapungia mikono Wageni mbalimbali waliofika katika hafla ya kuwaaga wastaafu hao iliyofnyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam Julai 21, 2017.
PIX 2
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakiwapungia mikono Wastaafu wa Jeshi la Magereza(hawapo pichani) katika hafla ya kuwaaga wastaafu hao iliyofnyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam Julai 21, 2017.
PIX 4
Baadhi ya askari wa Jeshi la Magereza wakifuatilia tukio la kuagwa wastafu hao kama inavyoonekana katika picha.
PIX 5
Naibu Kamishna Mstaafu wa Magereza, Edith Malya akisalimiana na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam, Naibu Kamishna wa Magereza, Augustine Mboje alipowasili katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam.
PIX 6
Naibu Kamishna Mstaafu wa Magereza, Edith Malya akikagua Gwaride maalum lililoandaliwa na Maofisa na askari wa Magereza kwa ajili ya kuwaaga wastaafu wa Jeshi hilo.
PIX 7
Gwaride maalum lililoandaliwa na Maofisa na askari wa Magereza kwa ajili ya kuwaaga wastaafu wa Jeshi la Magereza likipita mbele ya wastaafu wa Jeshi la Magereza kwa mwendo wa haraka.
PIX 8
Naibu Kamishna Mstaafu wa Magereza, Edith Malya akiwa jukwaa kuu wakati Gwaride likipita mbele kwa heshima.
PIX 9
Kamishna wa Fedha na Uatwala wa Jeshi la Magereza Gaston Sanga akisalimiana na Mnadhimu Msaidizi wa Jeshi la Magereza .Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Deogratis Lwanga (wa pili kulia) katika hafla ya kuwaaga wastaafu wa Jeshi hilo.
PIX 10
Kamishna wa Fedha na Uatwala wa Jeshi la Magereza Gaston Sanga (katikati) akifuatilia matukio ya kuagwa wastaafu wa Magereza, kulia ni  Mnadhimu Msaidizi wa Jeshi la Magereza Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Deogratis Lwanga na wa kwanza kushoto ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Mlasani Kimaro.

No comments