Header Ads

Responsive Ads Here

UZINDUZI WA FILAMU YA MAGWANGALA WAINGIA DOSARI


Naibu Waziri wa Habari Utamaduni ,Sanaa na
Michezo Mhe.Anastazia Wambura.Akizungumza juu ya kukwama kwa uzinduzi wa Filamu ya Magwangala ambayo imechezewa Mkoani Geita na wasanii pamoja na viongozi wa Serikali. 


Baadhi ya wadau wa Sanaa ya maigizo Mkoani Geita wakiwa kwenye Ukumbi wakisubilia hatima ya uzinduzi wa Filamu ya Magwangala.

Uzalendo wa kusubilia uzinduzi ndipo ulipowashinda wengine wakaamua waendelee kusakata Rumba uku wakisubilia taarifa ua uzinduzi majira ya saa sita za usiku.

Mzee wa Nguchu Kutoka  Desire Park
.
akiendelea kutumbuhiza kwenye uzinduzi wa Magwangala.

Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa kwenye ukumbi ambapo ndipo shughuli ilikuwa ikifanyika ya uzinduzi.

Mwenyekiti wa chama cha wasanii Mkoani Humo
ambaye pia ni moja kati ya wachezaji wa Filamu Hiyo ,Bi,Rosemery Michael(Rose Bonanza )Akielezea namna ambavyo wameweza kuingia hasara kutokana na uwandaaji wa filamu pamoja na uzinduzi.
Mbunge wa Geita,Mjini Constatine Kanyasu akielezea juu ya hatua ambayo imechukuliwa kwa kuzuiliwa kwa filamu ya Magwangala kuzinduliwa hadi pale itakapofanyiwa marekebisho.
 

Meneja Mahusiano ya Jamii wa Mgodi wa Geita,Manase Ndoroma akielezea kutokuwepo kwa ugomvi wa aina yoyote kati ya wasanii na mgodi wa GGM na hatua ambayo wameichukua baada ya kuonekana kuwepo kwa mahudhui ambayo yanaleta uchochezi baina ya wananchi na mgodi.

Baadhi ya wasanii ambao wameigiza kwenye filamu hiyo wakiwa nje ya ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Geita.
……………………………………………………
Uzinduzi wa Filamu ya Magwangala  ambayo imechezwa na wasanii wa Mkoani  Geita pamoja na
viongozi wa Halmashauri ya Mji   ulikuwa ufanyike siku jana (Julai 27) umekwama kutokana na kuwepo kwa madai ya mgodi wa dhahabu wa Geita(GGM) Kulalamika kuwa filamu hiyo inaonekana kuwa na mahudhui
ya  uchochezi baina ya wananchi na mgodi Mkoani humo.
 
Uzinduzi  huo ulitarajia kufanywa na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura Katika ukumbi wa Desire Park .
 
Akizungumza  juu ya hatua ya kukwama  kwa uzinduzi huo Naibu waziri  Wambura,amesema kuwa kilichotokea alipatiwa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa kwamba kuna picha ambayo sio nzuri na kwamba wao kama mgodi walilalamika juu ya picha hiyo na kwamba wameangalia na kuona kuwa kuna maeneo ambayo yamerekodiwa sio mazuri na tatizo ni mawasiliano baina ya Afisa utamaduni na Mkoa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha wasanii  Mkoani Humo ambaye pia ni moja kati ya
wachezaji wa Filamu Hiyo  Bi,Rosemery Michael ,amesema kuwa wao hawakuona mapungufu yoyote kwa maigizo ambayo wameigiza kwenye filamu hiyo ni uhalisia wa maisha ambayo yapo ndani ya Mkoa usika.
 
Baadhi ya wasanii na wananchi ambao wameudhuria siku ya jana kwenye uzinduzi wa Filamu Hiyo,Sagari Mganga na Neema Philipo wamesema kuwa hata wao wameshindwa kujua ni maswahibu gani ambayo yamejitokeza ambayo yamesababishwa filamu hiyo kutokuzinduliwa.
Manase Ndoroma ni meneja mwandamizi wa mgodi  ambaye anashughulika na maswala ya jamii, ndani ya Mgodi wa dhahabu wa Geita  (GGM)  amefafanua kuwa wao  hawana ugomvi na sanaa wala na wasanii ila kumetokea shida ambayo wametoa kwa jamii kwa makusudi na kwamba mgodi huo una athari kwa jamii ambayo inauzunguka.

No comments