Header Ads

Responsive Ads Here

TBL ILIVYOWASAMBAZIA RAHA YA MUZIKI VIJANA WA ILEJE


Burudani ileje 6
Izzo Business akitamba jukwaani katika  tamasha hilo 

Burudani ileje 2
Wasanii mbalimbali wakishiriki kumwaga moto wa burudani chini ya udhamini wa TBL
burudani ileje 17
Mbunge wa Ileje,Janeth Mbena (kulia) akibadilishana mawazo na Maofisa Waandamizi kutoka TBL wakati wa tamasha hilo la kukata na shoka.
………………………………….
Mwanamuziki  nguli wa muziki wa kizazi kipya Izzo Business, mwishoni mwa wiki alimwaga burudani kubwa kwa wakazi wa wilaya ya Ileje mkoani Songwe katika  bonanza la vijana na ujasiriamali ambalo lilifanyika katika kituo cha mabasi ya Itumba  likiwa limeandaliwa na mbunge wa jimbo hilo, Janeth Mbena, na kufadhiliwa na kampuni ya TBL.
Izzo Business aliweza kuwapagaisha washabiki wa muziki wa bongo  Fleva kutoka mwanzo wa onyesho hadi mwisho ambapo pia kulikuwepo burudani za kila aina kutoka wasanii mbalimbali chipukizi mkoani Mbeya na  kabla ya onyesho vijana walipatiwa mafunzo ya mbinu za ujasiriamali.
Mbunge wa jimbo hilo Janeth Mbena ambaye  alikuwa mgeni rasmi alisema kuwa lengo la tamasha hilo ni kuwaleta vijana pamoja kwa kuwapatia maarifa na mbinu za maisha ikiwemo  kuwaletea burudani na alitoa shukrani kwa TBL na wadau wengine kwa kulifanikisha.
Meneja Mawasiliano wa TBL Group,Zena Tenga ,akiongea udhamini huo alisema kuwa kampuni ya TBL Group kupitia moja ya sera yake ya ‘Kujenga Dunia Maridhawa’ imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha inatoa kipaumbele kudhamini michezo na burudani za muziki lengo likiwa ni kuleta burudani kwa jamii na kukuza vipaji vya wanamichezo na wasanii.
Tenga alisema  TBL imevutiwa na mkakati wa kuwapatia vijana elimu ya ujasiriamali ambao umeanza kutekelezwa wilayani Ileje.”Vijana ni kundi muhimu sana katika ukuzaji uchumi wa nchi hivyo wanahitaji kupata mbinu za kukabiliana na changamoto mbaimbali za maisha”.
Alimalizia  kwa kusema kampuni ya TBL nayo inatekeleza mpango wa kutoa elimu kwa wajasiriamali sambamba na kutoa elimu ya unywaji wa kistaarabu lengo likiwa  ni kujenga jamii ya watu makini ambao wanatumia vinywaji kwa ajili ya  afya na burudani na sio kwa ajili ya kuwa walevi na kuleta usumbufu kwenye  jamii.

No comments