Header Ads

Responsive Ads Here

TASMA WATANGAZA UCHAGUZI WA VIONGOZI WAO RASMI, UTAFANYIKA AGOSTI 5


tasma
Kutoka kushoto ni makamu mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Tasma, Francis Mchomvu, mwenyekiti wa kamati, Leslie Liunda, Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas na mjumbe wa kamati, Ombeni Zavara
Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Wataalamu wa Tiba za Michezo (Chawatimita-Tasma) imetangaza kuanza kwa mchakato wa uchaguzi wa chama hicho utakaofanyika Agosti 5, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Nafasi ambazo zinawaniwa ni mwenyekiti, makamu mwenyekiti, katibu mkuu, katibu mkuu msaidizi, mweka hazina, mjumbe wa mkutano mkuu TFF wajumbe wawili wa kamati ya utendaji.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Leslie Liunda, amesema kesho Julai 7, fomu zitaanza kutolewa katika ofisi za Tasma zilizopo kwenye Chama cha Paralympic zilizopo karibu na Uwanja wa Uhuru na mwisho ni Julai 16, mwaka huu.
“Gharama za fomu kwa wagombea wa nafasi ya wajumbe ni Sh 100,000, huku nafasi zingine gharama yake ikiwa ni Sh 200,000, fomu zitaanza kutolewa kila siku kuanzia saa 2 asubuhi mpaka saa 10 jioni,” alisema Liunda

No comments