Header Ads

Responsive Ads Here

TAARIFA YA JESHI LA POLISI KUTOKA MKOA WA MWANZA


msangii-1
TAREHE 10.07.2017 MAJIRA YA SAA 15:45HRS KATIKA BARABRA YA MWANZA KWENDA GEITA  ENEO LA NYAKAZUZU – KAMANGA TARAFA YA KATUNGURU WILAYA YA SENGEREMA MKOA WA MWANZA, GARI LENYE NAMBA T.618 BCU AINA YA SCANIA BUS  MALI YA KAMPUNI YA BUKWAYA LIKIENDESHWA NA DAEREVA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA DENIS SHILIWA @ SHIMBA, AMBAE ALITOROKA ENEO LA TUKIO BAADA YA AJALI KUTOKEA, LIKITOKEA MWANZA KWENDA CHATO MKOANI GEITA LILIACHA NJIA NA KUANGUKA CHINI NA KUSABABISHA VIFO VYA WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1.NGALAWA JUMA MIAKA 28, MKAZI WA USAGARA –MWANZA NA 2.RASHID KALEGA  MIAKA 22, UTINGO, MKAZI WA MWANZA NA KUSABABISHA  MAJERUHI KWA ABIRIA WATANO WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1.AMINA HUSSEIN MIAKA 27, MKAZI WA GEITA, AMBAE AMEVUNJIKA MKONO WA KUSHOTO, 2.MONIKA SHIJA MIAKA 48, MKAZI WA KIJIJI CHA KASAMWA, AMBAE AMEVUNJIKA MGUU WA KULIA, 3.IBRAHIM SIMON MIAKA 23, MKAZI WA MAHINA –MWANZA, AMEVUNJIKA MKONO WA KULIA, 4.JAMAL MICHAEL MIAKA 35, MKAZI WA RUNZEWE AMBAE AMEPATA MAUMIVU KIFUANI NA 5.JINA LAKE BADO HALIJAFAHAMIKA KWANI BADO HAJITAMBUI.

INADAIWA KUWA DEREVA WA GARI TAJWA HAPO JUUU ALIKUWA KWENYE MWENDO KASI NA PINDI  ALIPOFIKA KWENYE ENEO LA NYAKAZUZU –KAMANGA  GARI LAKE LILIPISHANA NA LORI LA MIZIGO AMBAPO DEREVA WA GARI HILO ALISHINDWA KULIMUDU GARI NA KUACHA NJIA NA KUSABABISHA GARI KUANGUKA CHINI NA KUSABABISHA VIFO VYA WATU TAJWA HAPO JUU NA MAJERUHI. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI NA UZEMBE WA DEREVA KUTOKUWA MAKINI WAKATI ALIPOKUWA BARABARANI.
POLISI WAPO KATIKA  MSAKO WA KUMTAFUTA DEREVA WA GARI HILO HADI ANAPATIKANA HUKU UCHUNGUZI KUHUSIANA NA TUKIO HILO UKIWA BADO UNAENDELEA. MAJERUHI WAMEPELEKWA HOSPITALI YA MISSION YA DDH YA MJINI SENGEREMA WAKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU NA HALI ZAO ZINAENDELEA VIZURI.  MIILI YA MAREHEMU PIA IMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO KWA AJILI YA UCHUNGUZI NA UTAMBUZI, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA ITAKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAENDESHAJI WA VYOMBO VYA MOTO HUSUSANI MADEREVA WA MABASI KUWA MAKINI PINDI WA WAWAPO BARABARANI HUKU WAKIZINGATIA KANUNI, SHERIA NA TARATIBU ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA MAJERUHI NA VIFO VINAVYOWEZA KUEPUKIKA.
KATIKA TUKIO LA PILI;
KWAMBA TAREHE 11.07.2017 MAJIRA YA SAA 03:00HRS USIKU KATIKA MTAA WA MAGAKA KATA YA KAHAMA WILAYA YA ILEMELA JIJI NA MKOA WA MWANZA, JENIFER SHEDAFA, MIAKA 32, MKAZI WA MAGAKA, ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMCHOMA TUMBONI MUMEWE AITWAYE HOSEA MAKOYE MIAKA 45, MFANYAKAZI WA TANESCO – MWANZA NA KITU CHENYE NCHA KALI KINACHOZANIWA KUWA NI KISU HADI AKAPOTEZA MAISHA, KITENDO AMBACHO NI KOSA LA JINAI.
INASEMEKANA KUWA WAWILI HAO WALIKUWA KWENYE UGOMVI WA MARA KWA MARA NDANI YA NDOA YAO, HALI ILIYOPELEKEA MWANAMKE KUWA NA TAMAA YA KUTAKA KURITHI MALI. INADAIWA KUWA MAJIRA TAJWA HAPO JUU WAKATI WAKIWA WAMELALA MWANAMKE ALIAMKA NA KUMVIZIA MUMEWE KISHA KUMCHOMA NA KITU CHENYE NCHA KALI TUMBONI NA KISHA KUJIPANGA KWA AJILI YA KUTOROKA ENEO LA TUKIO.
INADAIWA KUWA WAKATI MTUHUMIWA ANATEKELEZA TUKIO HILO MAJIRANI WALISIKIA KELELE ZA KUOMBA MSAADA HALI ILIYOPELEKEA KWENDA ENEO LA TUKIO NA KUWEZE KUMKAMATA MWANAMKE HUYO WAKATI ANATAKA KUTOROKA KISHA WAKATOA TAARIFA KITUO CHA POLISI. AIDHA ASKARI WALIFIKA ENEO LA TUKIO KWA WAKATI NA KUSHIRIKIANA NA WANANCHI KUMKIMBIZA MAREHEMU HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO LAKINI BAADAE MAREHEMU ALIFARIKI DUNIA WAKATI AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU, CHANZO CHA MAUAJI HAYO INADAIWA KUWA NI TAMAA YA MWANAMKE KUTAKA KURITHI MALI.
POLISI WAPO KATIKA UPELELEZI NA MAHOJIANO NA MTUHUMIWA, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA MTUHUMIWA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO KWA AJILI YA UCHUNGUZI, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA UTAKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.
KAMANDA WA POLISI MKAO WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KOSA LA JINAI, BALI PINDI WANAPOKUWA KWENYE MIGOGORO AIDHA YA NDANI YA NDOA AU YA AINA YOYOTE ILI WATOE TAARIFA POLISI, ILI POLISI WAWEZE KUTATUA MIGOGORO YA AINA KAMA HII KWA NJIA YA AMANI NA KUDHIBITI MAUAJI KAMA HAYA YASIWEZE KUTOKEA.
IMETOLEWA NA:
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

No comments