Header Ads

Responsive Ads Here

TAARIFA KUTOKA KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO JESHI LA ULINZI LA WANANCHI TANZANIA

JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO
Simu ya Upepo   : “N G O M E”                  Makao Makuu ya Jeshi,
Simu ya Mdomo : DSM 22150463              Sanduku la Posta 9203,
Telex                     : 41051                              DAR ES SALAAM,26Julai 2017
Tele Fax              : 2153426
Barua pepe       : ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
Tovuti                  : www.tpdf.mil.tz
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mkuu wa Majeshi ya India Admiral Sunil Lanba atawasili nchini kwa ziara ya kikazi. Mkuu wa Majeshi huyo atatembelea Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kuanzia saa 07:30 asubuhi. Atapokelewa kwa gwaride maalum lililoandaliwa na JWTZ katika viwanja vya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) vilivyopo  maeneo ya Upanga jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Majeshi huyo atakutana na kuongea na mwenyeji wake Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Venance Mabeyo ofisini kwake Upanga jijini Dar es Salaam.
Nyote mnakaribishwa katika mapokezi hayo.   
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203, Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi : 0756 716085

No comments