Header Ads

Responsive Ads Here

TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA


TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 06.07.2017.


Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kufanya misako, operesheni na doria zenye tija katika maeneo mbalimbali ili kudhibiti uhalifu na wahalifu na limekuwa likishirikiana na wananchi na wadau wengine katika jitihada hizo za kukabiliana na uhalifu na wahalifu na kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio makubwa ya uhalifu.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaongeza jitihada za kuzuia na kupunguza ajali za barabarani kwa kuhakikisha madereva na watumiaji wengine wa barabara wanatii sheria za usalama barabarani. Aidha kumekuwa na ajali 01 ya Vifo kama ifuatavyo:-

Mnamo tarehe 06.07.2017 majira ya saa 08:15 Asubuhi huko eneo la Mlomboji lililopo Kata ya Igawa, Tarafa ya Rujewa, Wilaya ya Mbarali Mkoa wa Mbeya katika Barabara ya Mbeya-Njombe, Gari yenye namba za usajili T.543 CSF aina ya HIGER Basi mali ya Kampuni ya Upendo lililokuwa likitokea Mbeya kuelekea Dar es Salaam likiendeshwa na Dereva aliyetambulika kwa jina la RAMADHANI MOHAMED [35] Mkazi wa Jijini Dar es Salaam liliacha njia, kupinduka na kusababisha vifo vya watu [abiria] wawili.
Abiria waliofariki katika ajali hiyo ni 1. EMANUEL OBED [30] Mkazi wa Chimala Mbeya na abiria mwingine aliyefahamika kwa jina moja la SHAIBU umri kati ya miaka 35 – 40.
Aidha katika ajali hiyo, abiria wanne walijeruhiwa ambao ni:-
  1. ESAU SANGA [43] Mkazi wa Makete
  2. FRANK NGIMBE [21] Mkazi wa Jijini Mbeya
  3. JENA MICHAEL [26] Mkazi wa Mbeya
  4. TUKUMBEKEGE MWAKYUSA [60] Mkazi wa Mbeya
Chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi. Dereva wa Basi hilo alikimbia mara baada ya ajali na juhudi za kumtafuta zinaendelea. Aidha Miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Mission Chimala. Majeruhi pia wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Mission Chimala na Rujewa.
WITO:

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishina Msaidizi wa Polisi AUGUSTINO I. SENGA anatoa wito kwa madereva kuwa makini wanapotumia vyombo vya moto ikiwa ni pamoja na kuzingatia sheria, alama na michoro ya usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika. Aidha Kamanda SENGA anaendelea kutoa wito kwa wananchi kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu kwa Jeshi la Polisi kwa hatua zaidi za kisheria.
                                            
                                             Imesainiwa na:
 [ACP – AUGUSTINO I. SENGA]
KAIMU KAMANDA WA POLISI
MKOA WA MBEYA

No comments