Header Ads

Responsive Ads Here

TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA  • MTU MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUJIFANYA DAKTARI WILAYANI MAGU.
MNAMO TAREHE 02/07/2017 MAJIRA YA SAA 21:00HRS USIKU KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MAGU ILIYOPO WILAYA YA MAGU MKOA WA MWANZA, EMMANUEL WILLIAM MIAKA 21, MKAZI WA MTAA WA ISANDULA – MAGU, ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUJIFANYA DAKTARI WA HOSPITALI YA WILAYA YA MAGU KISHA KUTAPELI WAGONJWA AKIWAOMBA WAMPATIE FEDHA ILI AWEZE KUWAPATIA HUDUMA YA MATIBABU, KITENDO AMBACHO NI KOSA LA JINAI.

INADAIWA KUWA MAJIRA TAJWA HAPO JUU MTUHUMIWA  ALIINGIA KWENYE WODI YA WANAUME HUKU AKIWA AMEVAA SURUALI NYEUPE NA GLOVES MIKONONI KISHA AKAJITAMBULISHA KWA WAGONJWA KWAMBA YEYE NI DAKTARI WA ZAMU. INASEMEKANA KUWA BAADA YA KUJITAMBULISHA ALIMFUATA MGONJWA MMOJA JINA TUNALIHIFADHI ALIYELAZWA WODINI HAPO KISHA AKAMWAMBIA AMPATIE TSH 100,000/, ILI AWEZE KUMFANYIA MPANGO WA KUPELEKWA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO KWA AJILI YA MATIBABU ZAIDI.
INASEMEKANA KUWA  BAADA YA MGONJWA KUELEZWA HIVYO ALIKUBALI NA KUMWOMBA MTUHUMIWA (DAKTARI FEKI) ASUBIRI HADI KESHO ASUBUHI YANI LEO TAREHE 03.07.2017, ILI AWEZE KUJA KUONGEA NA NDUGU ZAKE KUHUSU SUALA LA KUPELEKWA HOSPITALI YA BUGANDO NA KUMPATIA DAKTARI FEDHA ANAYOIHITAJI. INADAIWA KUWA BAADA YA NDUGU WA MGONJWA KUELEZWA SUALA HILO WALIPATA MASHAKA JUU YA DAKTARI HUYO KISHA WALITOA TAARIFA KWENYE UONGOZI WA HOSPITALI NA KITUO CHA POLISI.
POLISI KWA KUSHIRIKIANA NA UONGOZI WA HOSPITALI YA WILAYA MAGU WALIWEKA MTEGO, NA BAADAE POLISI WAKAFANIKIWA KUMKAMATA MTUHUMIWA, TAYARI MTUHUMIWA AMEFIKISHWA MAHAKAMANI KUJIBU TUHUMA ZA MASHITAKA YANAYO MKABILI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA HUSUSANI BAADHI YA VIJANA WENYE NIA OVU DHIDI YA TASNIA YA AFYA AKIWATAKA KUACHA TABIA HIYO MARA MOJA KWANI NI KOSA LA JINAI, NA MTU YEYOTE ATAKAYEKAMATWA AKIFANYA UDANGANYIFU WA AINA KAMA HII, HATUA STAHIKI ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA DHIDI YAKE.
IMETOLEWA NA;
DCP: AHMED MSANGI.
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

No comments