Header Ads

Responsive Ads Here

TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOA MWANZA


msangii-1TAREHE 10.07.2017 MAJIRA YA SAA 01:00HRS USIKU KATIKA KIJIJI CHA KIZUNGWANGOMA KATA YA MISSION WILAYA YA SENGEREMA MKOA WA MWANZA, MWANAMKE MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA BENADETA KULWA MIAKA 28, MKAZI WA KIJIJI CHA KIZINGWANGOMA, ALIMJERUHI KWA KUMKATA NA KITU CHENYE NCHA KALI MITHILI YA PANGA MUMEWE AITWAYE FRANCIS SHOMARI MIAKA 30, MKAZI WA KIJIJI CHA KIZUNGWANGOMA, KICHWANI NA NYUMA YA SHINGO WAKATI AKIWA AMELALA, KISHA NA YEYE KWENDA KUJINYONGA HADI KUFA KWA KUTUMIA KIPANDE CHA KANGA ALICHOKUWA AMEKIFUNGA KWENYE PAA LA NYUMBA, KITENDO AMBACHO NI KOSA LA JINAI.

INADAIWA KUWA WAWILI HAO WALIKUWA KWENYE MGOGORO WA NDOA WA MUDA MREFU, ULIOPELEKEA MWANAMKE KURUDI NYUMBANI KWA WAZAZI WAKE KUPUNZIKA, LAKINI JANA TAREHE 09/07/2017 MAREHEMU ALIRUDI KWA MUMEWE KUENDELEA NA MAISHA KAMA AWALI BAADA MGOGORO KUSULUHISHWA. INASEMEKANA KUWA WAKATI WAKIWA WAMELALA  USIKU MAJIRA TAJWA HAPO JUU MAREHEMU ALIAMKA NA KWENDA KUCHUKUA KITU CHENYE NCHA KALI MITHILI YA PANGA KISHA KWENDA KUMKATA MUMEWE KICHWANI NA NYUMA YA SHINGO. AIDHA INADAIWA KUWA BAADA YA KUFANYA KITENDO HICHO MAREHEMU ALIZANI KUWA TAYARI ATAKUWA AMEMUUA MUMEWE, NDIPO ALIAMUA KUCHUKUA MAAMUZI YA KWENDA KUJINYONGA HADI KUFA.
WANANCHI WALIFIKA ENEO LA TUKIO KUTOA MSAADA BAADA YA KUSIKIA KELELE ZA WATOTO WAKILIA, KISHA WALITOA TAARIFA KITUO CHA POLISI. ASKARI WALIFIKA ENEO LA TUKIO KWA WAKATI KISHA KUSHIRIKIANA NA WANANCHI KUMKIMBIZA MAJERUHI HOSPITALI YA MISSION YA DDH ILIYOPO MJINI SENGEREMA KUPATIWA MATIBABU NA HALI YAKE INAENDELEA VIZURI. CHANZO CHA TUKIO HILO INADAIWA KUWA NI WIVU WA KIMAPENZI KATI YA WAWILI HAO, HALI ILIYOPELEKA KUWEPO NA MGOGORO NDANI YA NDOA. MWILI WA MAREHEMU TAYARI UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA DAKTARI NA KUKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA HUSUSANI WANANDOA AKIWATAKA KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI PINDI WANAPOKUWA KWENYE MIGOGORO NDANI YA NDOA, BALI WAWATUMIE WAZEE WA FAMILI, WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA, VIONGOZI WA DINI, AU VYOMBO VYA DOLA ILI KUEPUSHA MATUKIO YA AINA KAMA HII YASIWEZE KUTOKE KWENYE JAMII ZETU.
IMETOLEWA NA:
DCP; AHMED MSANGI.
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

No comments