Header Ads

Responsive Ads Here

TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LEO

msangii-1
TAREHE 08.07.2017 MAJIRA YA SAA 05:00HRS ALFAJIRI KATIKA MTAA WA FUMAGILA MASHARIKI KATA YA IGOMA WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, MAJAMBAZI SITA AMBAO MMOJA AMEFAHAMIKA KWA JINA LA SELEMANI JUMA BAADA YA KUKUTWA NA KITAMBULISHO CHA KUPIGA KURA, HUKU WENZAKE WATANO WAKIWA HAWAJAFAHAMIKA MAJINA WAMEUAWA NA ASKARI POLISI KWA KUPIGWA RISASI SEHEMU MBALIMBALI ZA MIILI YAO, HII NI BAADA YA MAJIBIZANO YA KURUSHIANA RISASI KATI YA ASKARI POLISI NA MAJAMBAZI HAO NA KUPATIKANA KWA SILAHA MOJA AINA YA AK 47 YENYE NAMBA 1971E3445, SILAHA NYINGINE NNE (04) ZILIZOTENGENEZWA KIENYEJI, MAGAZINE MBILI ZA SILAHA YA AK 47 ZIKIWA NA RISASI 30 KILA MOJA, RISASI NYINGINE 36 ZA AK 47 ZILIZOKUWA ZIMEHIFADHIWA KWENYE BEGI, SARE ZA JESHI  ZINAZODHANIWA KUTUMIWA NA MAJESHI YA NCHI JIRANI PAMOJA NA MKANDA WAKE, KOFIA SITA ZA KUFICHA USO (MARSK) NA MABEGI MATATU YALIYOKUWA YAMEHIFADHI SILAHA, SARE ZA JESHI NA RISASI, PIKIPIKI MOJA YENYE NAMBA T.815 DAA AINA YA SANYA NA BAISKELI MBILI.

AWALI POLISI WALIPOKEA TAARIFA KUTOKA KWA WASIRI KWAMBA BAADHI YA WAHALIFU WANAOFANYA UHALIFU KATIKA MKOA WA PWANI KWENYE WILAYA YA KIBITI NA RUFIJI WAMEKIMBILIA MKOA WA MWANZA. KUTOKANA NA TAARIFA HIZO ASKARI WALIANZA KUFANYA UFUATILIA JUU YA TAARIFA HIZO KATIKA MAENEO MBALIMBALI YA JIJI NA MKOA WA MWANZA NA MAENEO JIRANI.
 AIDHA PIA ZILIPATIKANA TAARIFA KUWA MAJAMBAZI HAO NDIO WAOLIFANYA TUKIO LA UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA TAREHE 15.06.2017 KATIKA KIWANDA CHA KUTENGENEZEA MIKATE KIJULIKANACHO KWA JINA LA VICRORIA KILICHOPO NYAKATO  WILAYA YA NYAMAGANA MALI YA ABEID ABDULHAKIM @ ABEID MWARABU NA KUPORA FEDHA KIASI CHA MILIONI 30, KISHA KUKIMBILIA KUSIKO JULIKANA, AMBAPO ILIFUNGULIWA KESI YENYE NAMBA NY/IR/4747/2017.
KATIKA UFUATILIAJI ALIKAMATWA MTUHUMIWA MMOJA AMBAYE KATIKA MAHOJIANO ALIKIRI KUHUSIKA KATIKA TUKIO TAJWA HAPO JUU LA UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA, KISHA ALITOA USHIRIKIANO KWA ASKARI AMBAPO ALIWAPELEKA ASKARI HADI ENEO LA FUMAGILA AMBAPO ALIDAI KUWA WENZAKE WAMEJIFICHA. NDIPO ASKARI WALIPOFIKA ENEO HILO GHAFLA MAJAMBAZI HAO WALIKURUPUKA NA KUANZA KUWARUSHIA ASKARI RISASI, AIDHA KUTOKANA NA UMAHIRI WA ASKARI WALIWEZA KUJIBU MASHAMBULIZI NA KUWEZA KUFANIKIWA KUWAUA MAJAMBAZI SITA HUKU WENGINE WAWILI WAKIFANIKIWA KUTOROKA ENEO LA TUKIO NA KUFANIKIWA KUPATIKANA KWA SILAHA TAJWA HAPO JUU, RISASI NA VITU VINGINE, UFUATILIAJI WA KUWASAKA HADI KUWATIA NGUVUNI WALE WALIOTOROKA BADO UNAENDELEA. AIDHA HAKUNA ASKARI ALIYEJERUHIWA KWA RISASI AU KUPOTEZA MAISHA KATIKA TUKIO HILO.
KAMANDA WAPOLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI WOTE WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWAOMBA KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI KWA KUTOA TAARIFA ZA UHALIFU NA WAHALIFU WA AINA KAMA HII MAPEMA ILI WAWEZE KUKAMATWA NA KUFIKISHWA KWENYE VYOMBO VYA SHERIA. AIDHA PIA ANAWASIHI VIJANA KUACHA TABIA YA KUJIHUSISHA NA UHALIFU WA AINA KAMA HII KWANI WATAWEZA KUINGIA KWENYE MATATIZO KAMA HAYA WALIYOYAPA WENZAO, PIA ANAONGEZA KUWA OPERESHENI YA AINA KAMA HII YA KUWASKA WALE WOTE WANAOJIHUSISHA KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE KWENYE MATUKIO YA UHALIFU KUWA NI ENDELEVU.
IMETOLEWA NA;
DCP: AHMED MSANGI.
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

No comments