Header Ads

Responsive Ads Here

SWAT Team kuelimisha jamii kuelewa ugonjwa wa Usonji (Autism)


ARTISM 2
Mmoja wa wanafunzi waliohudhuria hafla ya kuchangisha pesa, kwa ajili ya kuwasaidia watoto wenye matatizo ya ugonjwa wa Autism iliyoandaliwa na  Swat Team, Obrien Justee, akitoa burudani

ARTISM 3
Mratibu wa SWAT Team, Kemilembe Mugangala,akizungumza katika hafla ya kuchangisha pesa kwa ajili ya kuwasaidia  watoto wenye matatizo ya ugonjwa wa Autism iliyofanyika jijini Dar es Salaam
ARTISM
Msanii na Mwanamitindo , Frank Maston, akitoa burudani  wakati wa hafla hiyo.
…………………………………………………………………………….
• Familia nyingi Tanzania hazina ufahamu wa hali hii
Kikundi cha baadhi ya wanafunzi wanaosoma sekondari na vyuo vikuu nchini na nje wameanzisha  taasisi ijulikanayo kama Stand With Autism Tanzania (SWAT Team )inayolenga kuelimisha umma kuhusu ugonjwa wa usonji (Autism),unaoathiri zaidi watoto ambao watanzania wengi hawaufahamu.

Mratibu wa taasisi hiyo ,Kemilembe Mugangala,alisema mwishoni mwa wiki wakati wa hafla ya kufanikisha lengo hilo iliyofanyika katika klabu ya Woodberry CafĂ© jijini Dar es Salaam kuwa wamelenga zaidi kuelimisha jamii ili iweze  kuelewa ugonjwa huu na kuacha kuwanyanyapaa waathirika wake
Mugangala alisema SWAT Team wamebaini kuwa licha ya kuwepo na changamoto za magonjwa mengi nchini yapo ambayo hayajulikani vizuri kwenye jamii kama ulivyo ugonjwa huu wa Usonje ambapo yanaacha kundi la waathirika wake na familia  zako kuteseka  bila  kujua nini cha kufanya na ndio maana wamepania kuendesha kampeni kwa jamii dhidi yake.

“Ugonjwa wa usonje hautokani na laana au ushirikina kama jamii nyingi zinavyoamini  na jamii nzima hususani wakazi wa maeneo ya vijijini wanapaswa kulielewa hilo na kujua jinsi ya kuwasaidia watoto wenye tatizo hili badala ya kuwaficha majumbani na kuwaacha bila kuwapatia msaada utakaowasaidia kumudu maisha yao ya baadaye”. alisema Mugangala

Kuhusu mkakati watakaotumia kuendesha kampeni zao alisema watafanya kazi kwa  kushirikiana na wataalamu wa afya ambapo  kupitia mtandao wao watatembelea familia zilizoathirika na tatizo hili na kuzipatia ushauri wa kuwasaidia watoto hawa ikiwemo kufanya semina kwa wananchi hususani maeneo ya vijijini na kampeni mbalimbali kupitia vyombo vya habari kuhusiana dalili za ugonjwa na jinsi ya kuwasaidia waathirika wake kupata matibabu yake au kuishi nao
Alibainisha kuwa  ukosefu wa  ufahamu wa tatizo hili  husababisha watoto wengi wenye ugonjwa huo kupata mateso makubwa ya kupigwa sana,kutengwa kwa kufungiwa ndani na mateso mengine wakijua ni utundu wa mtoto.

Baadhi  ya dalili za ugonjwa huo ambao huadhimisha kidunia tarehe 2 Aprili ni mtoto kushindwa kuwatazama watu machoni,kushindwa kuongea na hutumia vitendo au picha kueleza mahitaji yake,kutoelewa wanachosema,kurudiarudia wasemacho watu wengine,kupenda kukaa peke yake,kucheza mchezo mmoja kila siku au kutumia kitu anachokipenda kukishika kila siku na kucheza nacho kila siku.

Wataalamu wa afya duniani hawajaweza kubaini chanzo cha ugonjwa huo kwa watoto lakini tatizo hilo huanza kuonekana kwa mtoto pale anapofikisha umri wa miaka mitatu ambao ndio umri mtoto anatakiwa kuanza kuonyesha uwezo wake wa kutambua vitu,kuiga tabia na kujifunza vitu mbalimbali

No comments