Header Ads

Responsive Ads Here

SPIKA WA BUNGE APOKEA MSAADA WA MIFUKO 200 YA SARUJI NA HUNDI YA SH. MILIONI 15 KUTOKA BENKI YA CRDB TAWI LA DODOMA KWA AJILI YA UJENZI WA NYUMBA ZA WALIMU, WILAYANI KONGWA, DODOMA.


unnamed
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai  (katikati) akipokea   hundi ya shilingi  milioni 15 na msaada wa  Mifuko mia mbili (200) ya sementi kutoka   kwa Mkurugenzi wa CRDB Benki Tawi la Dodoma Ndg. Rehema Hamisi  (kushoto) waliotoa ili kusaidia ujenzi wa nyumba za Walimu  wa Shule ya sekondari Laikala iliyopo Wilayani Kongwa, Dodoma. Wengine katika picha ni wafanyakazi wa Benki hiyo tawi la Dodoma.

1
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (katikati) akionyesha  hundi ya shilingi  milioni 15 aliyokabidhiwa na Mkurugenzi wa CRDB Benki Tawi la Dodoma Ndg. Rehema Hamisi (kushoto) alipokuwa wanatoa msaada wa ujenzi wa nyumba za Walimu  wa Shule ya sekondari Laikala iliyopo Kongwa, Dodoma kulia  ni Mkuu wa Shule hiyo Ndg. Msafiri Simon.
2
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza mara baada ya kukabidhiwa    hundi ya shilingi  milioni 15 na Mkurugenzi wa CRDB Benki Tawi la Dodoma Ndg. Rehema Hamisi alipokuwa wanatoa msaada wa ujenzi wa nyumba za Walimu  wa Shule ya sekondari Laikala, Kongwa, Dodoma. Walioshikilia hundi hiyo ni Wanafunzi wa shule hiyo.
3
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Walimu, Wanafunzi wa shule ya Laikala iliyopo Kongwa, Dodoma na wakazi Kata ya Saranga (hawapo pichani), mara baada ya kupokea msaada huo kushoto ni Mkurugenzi wa CRDB Benki Tawi la Dodoma Ndg. Rehema Hamisi na kulia Diwani wa kata ya Sagara Ndg. Simon Kamando.
(Picha na Ofisi ya Bunge)

No comments