Header Ads

Responsive Ads Here

SHIRIKA LA BIMA LA TAIFA NIC LAENDELEA KUTOA HUDUMA KWA WATEJA WAKE KWENYE MAONYESHO YA SABASABA JIJINI DAR ES SALAAM


01
Afisa Mauzo wa Shirika la Bima la Taifa NIC Bw. Vicent Rogath akipokea fedha kutoka kwa Askari wa Usalama Barabarani Afande Kudra Mbura baada ya kukata bima ya magari yake mawili kwa shirika hilo la taifa la Bima kwenye viwanja vya maonyesho ya biashara ya Sabasaba yanayofanyika  kwenye viwanja vya Mwalimu J. K. Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam kila mwaka kuanzia mwezi wa saba, Maonyesho hayo yanaandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara ya Nje (TANTRADE) kushoto ni Afisa wa Bima Bi. Janeth Kalinga.

1
Afisa Mwandamizi wa Bima Bw. Jumanne Nyamgunda akitoa maelezo kwa wananchi waliofika kwenye banda la shirika hilo ili kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na shirika hilo katika maonyesho ya sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu JK. Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam
2
Afisa Mwandamizi wa Bima Bw. Jumanne (NIC) Nyamgunda akitoa maelezo kwa Dk. Ramesh Shah aliyekuwa Jaji Mkuu wa Kamati ya Miss Tanzania wakati alipotembelea banda la shirika hilo.
3
Wafanyakazi wa Shirika la Bima la Taifa NIC wakiwa katika picha ya pamoja kwenye banda lao lililopo kwenye banda kuu la Wizara ya Fedha na Mipango.
5
Wafanyakazi wa Shirika la Bima la Taifa NIC wakiwa katika picha ya pamoja kwenye banda lao lililopo kwenye banda kuu la Wizara ya Fedha na Mipango.

No comments