Header Ads

Responsive Ads Here

Sera ya fursa sawa za jinsiaTBL Group yapongezwa na viongozi wa vyama vya wafanyakazi kutoka Zambia


Tico tour 4
Ujumbe wa wageni wakiangalia bia zinavyotengenewa kiwandani
Tuico tour 7
Meneja Mawasiliano wa TBL Group,Zena Tenga akielezea ujumbe  miradi mbalimbali ya kijamii ya kampuni
tuico tour 1
Mtaalamu wa upishi wa bia wa TBL Group, Roseana Modest,akiupatia ujumbe huo maelezo kuhusiana na mchakato wa kutengeneza bia
tuico tour 2
Ujumbe wa wageni na maofisa wa TBL Group katika picha ya pamoja baada ya ziara
Tuico tour 6
Mtaalam wa Ubora wa kiwanda cha bia cha TBL Jane Mwambuma (kushoto) akiwapa maelezo ya utengenezaji bia wageni waliotembelea kiwanda
……………………………………………………………………………….
Viongozi wa wanawake wa  Vyama vya  wafanyakazi kutoka  nchini Zambia na  viongozi wanawake wa  vyama vya  wafanyakazi kutoka nchini (TUICO)  wamefanya ziara ya mafunzo katika kiwanda cha TBL kilichopo jijini Dar es Salaa na wamevutiwa na mkakati wa kampuni hiyo wa kuzingatia usawa wa jinsia kwa kutoa fursa sawa za uongozi ndani ya kampuni ikiwemo jitihada za kuwakwamua wanawake wasio waajiriwa kiuchumi katika utekelezaji wa sera ya kampuni mama ya ABInBev ya ‘Dunia Maridhawa’.
Akiongea na ujumbe wa wanawake hao,Meneja Mawasiliano wa TBL Group,Zena Tenga, alisema mkakati huo wa kuzingatia usawa wa kijinsia unachangia kwa kiasi kikubwa kampuni hiyo kuendelea kupata mafanikio makubwa katika nyanja mbalimbali.
Zena Tenga, alisema kuwa kampuni  inatekeleza kwa vitendo sera ya kampuni yake mama ya kimataifa ya ABInBev ambayo inatoa fursa sawa kwa wafanyakazi wake wote bila kujali jinsia ikiwemo kuwapatia fursa za uongozi  wafanyakazi wanawake ndani ya viwanda vyake na sehemu nyinginezo za biashara zake na wanaendelea kufanya vizuri na kudhihirisha kuwa ujuzi hauna jinsia.
Alisema kampuni inalo jukwaa la wafanyakazi wanawake walioajiriwa na kampuni lijulikanalo kama TBL Women’s Forum  ambalo lengo lake kubwa ni kuwaunganisha wafanyakazi wote wanawake ndani ya kampuni na kuwawezesha kubadilishana mawazo ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za kimaisha ikiwemo kuweka mikakati ya kujiendeleza katika fani zao.
“Pamoja na kuzingatia usawa wa kijinsia kampuni inao mkakati wa kuwaendeleza wafanyakazi wanawake kielimu ambapo tayari baadhi ya wafanyakazi  wamewezeshwa kuhudhuria na wamehitimu mafunzo ya ‘Mwanamke wa Wakati ujao’  yanayotolewa na na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa kushirikiana na taasisi ya Confederation of Norwegian Enterprises (NHO)”alisema.
Tenga aliueleza ujumbe huo mafakio mbalimbali ambayo kampuni imepata ikiwemo kupata tuzo mbalimbali ikiwemo tuzo ya mwajiri bora nchini na tuzo ya kimataifa ya Top Employers Award kutokana na utekelezaji wa kanuni za raslimali watu kwa viwango vinavyokubalika kimataifa vilevile kutekeleza miradi ya kuwasaidia akina mama kjikwamua kiuchumi mojawapo ukiwa ni mradi wa Chibuku Mamas.
Akiongea kwa niaba ya wenzake,Brenda Mufika kutoka Chama cha wafanyakazi Migodini nchini  Zambia, alisema wamejifunza mambo mengi katika ziara yao kiwandani hapo na moja ya suala kubwa lililowavutia ni kampuni kuzingatia usawa wa kijinsia katika maeneo ya kazi,kuzingatia sheria za kazi za nchi pia kufanya uzalishaji wa kutumia teknolojia za kisasa na rafiki kwa mazingira na uzingatiaji wa hali ya juu wa kanuni za usalama mahali pa kazi.
Mufika alitoa wito kwa taasisi mbalimbali kuwapatia wanawake nafasi ya kupata mafunzo  ya kuwawezesha kushika nafasi za uongozi wa juu katika sehemu zao za kazi  na kwenye vyama vya kutetea maslahi ya wafanyakazi kwa kuwa dunia ya sasa inahitaji elimu ya kisasa katika kukabiliana na changamoto mbalimbali na kuleta ufanisi katika sehemu za kazi

No comments