Header Ads

Responsive Ads Here

RC TABORA NUNUENI PAMBA KWA BEI YA 1,500/- ILI KUPATA MALIGHAFI YA KUTOSHA KUZALISHA NYUZI.

 
Na Tiganya Vincent,RS-TABORA
27 July 2017

Mmiliki wa Kiwanda cha Nyuzi cha Tabora ametakiwa kuongeza wa bei ya ununuzi wa pamba kutoka shilingi 1,000/ – hadi 1,500/- kwa ajili ya kuwavutia wakulima wengi kupeleka bidhaa yao na hivyo kuwa  na malighafi ya kutosha katika uzalishaji wa nyuzi na kamba kwa matumizi mbalimbali.

Kauli hiyo imetolewa jana mjini Tabora na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri aliyeongoza Kamati ya Ulinzi na Usalama kwa ajili ya kutembelea Kiwanda hicho ili kuangalia halisi ya utendaji wa Kiwanda na kutoa ushauri wa kuboresha utendaji wao.
Bw. Mwanri aliongeza kuwa upatikanaji wa pamba kwa wingi kwa ajili ya Kiwanda hicho na uzalishaji wa nyuzi na kamba ambazo zina viwango bora utawasaidia  wao kuhimili ushindani katika masoko mbalimbali na hivyo kutengeneza ajira kwa vijana mbalimbali na kuongeza mapato ya Serikali.
Alisema kuwa kikanza kuzalisha kwa wingi bidhaa mbalimbali  kitakifanya Kiwanda hicho kuwa kuepuka majengo yake kugeuka kama maghala ya kuhifadhi bidhaa kama wanavyofanya baadhi ya watu waliobinafusishiwa Viwanda hapa nchini.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa huyo amemtaka Mmiliki wa Kiwanda hicho kupeleka nakala ya Mkataba uliosainiwa wakati wa Ubinafishaji ili kuona kama anazingatia masharti ya ununuzi wa Kiwanda hicho.
Aliongeza kuwa upo uwezekano wa kuwepo maeneo ambavyo yapo katika Mkataba huo lakini bado mmunuzi huyo hajatekeleza na ndio sababu ya kususua kwa kiwanda hicho.
Naye Mkurugenzi wa Kiwanda Mtendaji wa Kiwanda cha Nyuzi Tabora Urveshi Rajani alisema kuwa yuko tayari kununua pamba yote ya wakulima wa Mkoa wa Tabora endapo atahakikishiwa upatikanaji wa soko la bidhaa zao kama nyuzi ikiwemo wakulima wa tumbaku kupitia Chama cha Ushiriki cha Wakulima wa Tumbaku(WETCU) kununua.
Alisema kuwa kama WETCU wataamua kununua nyuzi zao wako tayari kuhakikisha kuwa pamba yote inayolimwa mkoani Tabora watanunua kwa bei nzuri na kuendelea kuboresha bei kulingana na wanavyouza bidhaa zao.
Aidha Mkurugenzi huyo Mtendaji alitoa wito kwa Serikali kudhibiti uuingazaji kinyemela wa bidhaa kutoka nje kama vile Khanga ambayo zinzalishwa nje lakini zinaandikwa kuwa zimetengezwa Tanzania , hali inayochangia kudhofisha Viwanda nchini.
Kwa upande wa Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Dkt. Thea Ntara alitoa wito Watendaji wote kuhakikisha wanasimamia wakulima wanazalishe pamba ya kutosha kwa ajili ya kukiwezesha kiwanda hicho kuwa na malighafi ya kutosha ili kuzalisha nyuzi za kutoa.
Aliongeza kuwa wanapaswa kuwasimamia wakulima ili wazalishe pamba ambayo itakuwa safi na itamvutia Mmiliki wa Kiwanda hicho kununua kwa wingi na kutoa bei ya juu zaidi.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Tabora Queen Mlozi alitoa wito kwa wazalishaji wa mazao mbalimbali ikiwemo tumbaku, korosho na kahawa kununua nyuzi za Kiwanda cha Tabora ili kuunga mkono juhudi za Mwekezaji huyo na kumsaidia ili uzalishaji wake utakapoongezeka atatoa ajira kwa vijana wengi.
Aliongeza kuwa wale wanahitaji nyuzi kwa ajili ya utengenezaji wa nguo mbalimbali wanatakiwa kununua za Kiwanda hicho ili kumuunga mkono mwekezaji huyo.
Kiwanda cha Nyuzi Tabora hivi sasa kinao watumishi 24 badala ya 350 waliokuwepo hapo awali.

No comments