Header Ads

Responsive Ads Here

RC MAKONDA AKABIDHIWA WINGLE 5


MAKO2
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda leo asubuhi amekabidhiwa zawadi ya gari aina ya Double Cabin Wingle 5 kutoka kwa kampuni ya watengenezaji wa magari ya  Great Wall Motor Company ya Afrika Kusini ikishirikiana na kampuni ya wauzaji Magari ya Kifaru Motors ya Tanzania.

Akiongea katika makabidhiano hayo mkurugenzi wa Great Wall Motor Company ukanda wa Kusini mwa Afrika Bwana Jianguo Liu alisema kuwa zawadi hiyo ni ishara ya kampuni hiyo kutambua jitihada mbalimbali  za ofisi ya mkuu wa Mkoa na watumishi wake wanazofanya katika kutumikia wananchi na kusaidia kuboresha utendaji kazi.
Katika salamu za shukrani Mh. Makonda alishukuru uongozi mzima wa kampuni ya Great Wall ukishirikiana na wauzaji Kifaru Motors kwa kutambua jitihada za ofisi yake na kuahidi kuendelea kuwatumikia wananchi wa Dar es salaam kwa moyo na kutimiza falsafa ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mh. Dr John Pombe Magufuli ya “HAPA KAZI TU”.
Mkuu wa Mkoa ameahidi kuwa gari hilo litatumika ipasavyo katika kuwahudumia wananchi wa Dar es salaam kutumia idara itakayoonekana kuwa ndio Mtoa huduma bora katika Mkoa wa Dar es salaam.
“Naomba kuitoa hii gari kama Zawadi kwa Idara inayohudumia vizuri wananchi wangu na ili nitoe kwa idara hiyo naomba wananchi wenyewe watutumie kwa ujumbe mfupi kupitia namba tutakayoitangaza . Kazi ya mwananchi ni kusema tu idara hii inawahudumia vizuri wanapofika kwenye ofisi zao, kama ni Afya,elimu,Ardhi,Biashara na Mahakama.” Aliongeza Makonda.
Kwa mfano kama ulienda idara ya Elimu, Ardhi, Afya au Biashara ukapewa huduma nzuri katika eneo mojawapo kati ya hayo unachotakiwa ni kutuma meseji fupi inayoonyesha idara hiyo ili wapewe zawadi hiyo ya Gari kama motisha waendelee kutoa huduma nzuri.
Utaratibu wa kutuma ujumbe huo wa kuchagua idara bora katika utendaji utatolewa kupitia namba maalum ambayo itatolewa hapo baade.

No comments