Header Ads

Responsive Ads Here

Rais wa ABInBev Afrika Ajionea TDL Ilivyojipanga Kufanya Uzalishaji Usio na Athari Kwa Mazingira


unnamed
Mkurugenzi wa TBL Group,Roberto Jarrin (kushoto) akibadilishana mawazo na Rais wa ABinBev kanda ya Afrika,Ricardo Tadeu,wakati alipofanya ziara ya kikazi katika kiwanda cha Konyagi (TDL) kilichopo jijini Dar es Salaam,wengine pichani wa kwanza kulia ni Meneja ubora wa kiwanda hicho, Asheri Magandi  na Mhandisi Mwandamizi wa kiwanda hicho,Salvatory Rweyemamu.

1
Rais wa ABInBev Africa,Ricardo Tadeu (wa pili kulia) akipata maelezo jinsi mtambo mpya wa kuzalisha vifungashio vya vioo unavyofanya kazi kutoka kwa Meneja Ubora wa kiwanda cha Konyagi,Asheri Magandi wakati alipofanya ziara ya siku moja nchini jana.Wengine pichani ni Maofisa waandamizi wa kiwanda hicho kilichopo jijini Dar es Salaam
2
Rais wa ABInBev Africa,Ricardo Tadeu akitembelea eneo la mtambo wa vifungashio vya kioo wa TDL na kupatiwa maelezo kuhusiana na uzalishaji
……………………
 
Ni utekelezaji wa sera ya kampuni ya Better World
 
Rais wa kampuni ya mama ya TBL ya ABInBEV kanda ya Afrika,Ricardo Tadeu, amefanya ziara ya siku moja nchini na kutembelea kiwanda cha TDLmaarufu kama Konyagi kilichopo jijini Dar es Salaam ambapo alijionea jitihada za kiwanda hicho kufanya uzalishaji kwa kufuata  kanuni za utunzaji wa mazingira.
 
Tadeu pia alipata fursa ya kutembelea mtambo mpya wa kuzalisha vifungashio vya  vinywaji vya kioo badala ya mifuko ya plastiki ukiwa ni utekelezaji wa agizo la serikali la kupiga marufuku kuuza vinywaji vilivyofungwa kwa kutumia mifuko ya plastiki maarufu kama viroba.
 
Mkurugenzi wa TBL Group na Mkuu wa Masoko kanda ya Afrika Mashariki,Roberto Jarrin,alieleza jinsi TBL Group  ilivyojipanga kutekeleza kwa vitendo mkakati wa serikali ya awamu ya tano wa kuifanya Tanzania kwa nchi ya viwanda sambamba na kuendesha viwanda kwa kutumia teknolojia za kisasa ambazo ni rafiki kwa mazingira.
 
Tunafurahi kuona serikali ya awamu ya tano inaweka msisitizo wa kujenga viwanda nasi kama wawekezaji katika sekta hii tumejipanga kuendelea kuwa na viwanda bora vinavyotumia teknolojia za kisasa na rafiki kwa mazingira,kupunguza matumizi ya maji,kupanua wigo wa ajira kwa kufanya kazi kwa kushirikiana na wakulima wanaotuuzia malighafi na kuchangia pato la serikali kwa kulipa kodi”.Alisema Roberto.
 
Roberto alieleza kuwa hivi sasa kampuni ya TDL ambayo iko chini ya TBL Group imefunga mtambo wa kisasa wa kuzalisha vifungashio vya kioo ambao utawezesha vinywaji vilivyokuwa vinafungwa kwenye vifungashio vya plastiki kupatikana kwenye vifungashio vya kioo vyenye ubora,rafiki wa mazingira na ambavyo sio rahisi kuigizwa na wafanyabiashara wasio waaminifu kwenye masoko.
 
Mkurugenzi huyo wa TBL Group alimhakikishia Rais huyo wa ABInBEV kuwa itahakikisha inafanya kazi kwa kushirikiana na serikali na wadau wote kuhakikisha mkakati wa kufanya mapinduzi ya viwanda nchini unapata mafanikio na kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta hii.

No comments