Header Ads

Responsive Ads Here

RAIS MAGUFULI APATA MAPOKEZI MAKUBWA GEITA

Rais Dkt.John Pombe Magufuli jana ewasili mkoani Geita na kulakiwa na mamia ya wananchi waliokuwa wamejipanga barabarani. Akisalimiana na wananchi mjini Geita, Rais Magufuli amepiga marufuku suala la kuwanyanyasa wachimbaji wadogo wa dhahabu katika maeneo yao.
Rais Magufuli amesema kwake yeye wachimbaji wadogo ndiyo wakubwa, na wale wakubwa kwake ndio wadogo na hivyo kutaka hao wachimbaji wadogo wasisumbuliwe.
Rais Magufuli aliwasili jana mkoani Mwanza ambapo juzi amefanya uzinduzi wa mradi mkubwa wa maji katika eneo la Nyamazugo wilayani Sengerema wenye thamani ya shilingi bilioni 23 ambao utamaliza kilio cha maji walichokuwa nacho wakazi wa Sengerema kwa muda mrefu.

Habari zaidi bonyeza HAPA 

No comments