Header Ads

Responsive Ads Here

NMB yadhamini mashindano ya Golf Gymkhana Dar

Meneja Mahusiano ya Wateja wa NMB, Gibson Mlaseko akimkabidhi tuzo ya ushindi wa mchezo wa Golf, Samwel Mosha katika michuano ya mchezo huo maalumu kwaajili ya kuadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Clabu ya Gymkhana ya jijini Dar es Salaam. Benki ya NMB ilidhamini mashindano hayo yaliyofanyika kwa siku mbili na kushirikisha wanamichezo mbalimbali.


 BENKI ya NMB imedhamini mashindano ya mchezo wa Golf yaliyoandaliwa na Club ya Gymkhana ya jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 100 tangu kuanzishwa kwa club hiyo. Michuano hiyo mikali na ya kipekee iliyopambanisha wachezaji wa mchezo wa golf kutoka club mbalimbali ilifanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam na washindi mbalimbali wa mchezo huo kujishindia tuzo baada ya kuibuka kidedea hatua mbalimbali. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe ndiye mgeni rasmi aliyewaongoza wageni mbalimbali waalikwa kwenye hafla ya kuwakabidhi tuzo washindi kabla ya kuyapongeza makampuni mbalimbali ikiwemo Benki ya NMB iliyofanikisha michuano hiyo.
  Menaja Mahusiano ya Wateja wa NMB, Gibson Mlaseko akimkabidhi tuzo ya ushindi wa mchezo wa Golf, Bi. Tayana William katika michuano ya mchezo huo maalumu kwaajili ya kuadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Clabu ya Gymkhana ya jijini Dar es Salaam. Benki ya NMB ilidhamini mashindano hayo yaliyofanyika kwa siku mbili na kushirikisha wanamichezo mbalimbali.

Katika hafla hiyo ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa mchezo wa golf, NMB ilipata fursa ya kukabidhi tuzo sita kwa washindi mbalimbali, wakiwemo; Samwel Mosha, Chiku Eliasy, Tayana William, Eric Tango, Vicky Elias pamoja na Mohamed Rahim aliyetwaa tuzo ya mshindi wa Jumla wa mchezo huo. Hata hivyo, katika hafla hiyo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe pia aliikabidhi Benki ya NMB na makampuni mbalimbali tuzo ya shukrani iliyotolewa na Uongozi wa Club ya Gymkhana ya jijini Dar es Salaam kutambua mchango wa benki hiyo na taasisi zingine katika mafanikio ya mchezo wa Golf.

No comments