Header Ads

Responsive Ads Here

NGOMA MBICHI MALINZI, MWESIGWA WAKOSA TENA DHAMANA, WARUDISHWA RUMANDE


Malinzi na Mwesigwa walifikishwa leo mahakamani Kisutu kwa mara ya pili na kurejeshwa rumande hadi kesi yao itakaposikilizwa kwa mara nyingine Julai 17, mwaka huu.
Wawili hao wanakabiliwa na mashitaka mbalimbali kuanzia 25 hadi 28 likiwemo lile la matumizi mabaya ya ofisi na utakatishaji wa fedha.
Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Wilbard Mashauri  alisema upande wa utetezi wenyewe wanatambua kuwa mashitaka ya utakatishaji fedha hayana dhamana.

No comments