Header Ads

Responsive Ads Here

NAPOMUONA DIDIER DROGBA MPYA KWENYE SURA YA LACAZETTE


420F92BD00000578-4667062-image-m-2_1499326324004
ABDUL DUNIA
KARIBU Arsenal Alexandre Lacazette. Karibu kwenye timu iliyoweka historia ya kuuchukua ubingwa wa England bila ya kufungwa.

Karibu sana London Alexandre. Tusipokukaribisha sisi mashabiki wanazi wa Arsenal nani mwingine wakukukaribisha?
Unapokuja London Alexandre jua kuna timu moja ya kuitumikia nayo ni Arsenal. Timu ambayo waliwahi kucheza wachezaji wengi kutoka Ufaransa na wakan’gara. Timu ambayo kocha wake ana historia ya kupewa jina la ‘Invicible Coach’ yaani kocha asiyefungika. Bahati iliyoje hiyo Alecandre.
Bahati ya kufundishwa na kocha asiyefungika. Bahati ya kucheza katika timu isiyofungika. Timu iliyoifunga Real Madrid iliyosheheni mastaa hakuna mfano wake duniani ‘Galacticos’. Hakika Madrid walikaa pale Emirates.
Madrid iliyoongozwa na Zinedine Zidane, Ronaldo De Lima, Raul Goinzalez, David Bekham, Guti H., Roberto Carlos na wachezaji wengi wa dunia. Ilikubali kichapo toka kwa Arsenal ya wanaume iliyokuwa ana akina Jens Lehman, Thierry Henry, Pires, Reyes, Fabregas, Campbel na wengi wengine. Karibu Lacazette.
Lacazette ni moja ya washambuliaji hatari duniani ‘world class player’ timu yake pekee aliyokuwa akiitumikia ndio iliyokuwa kikwazo kwako. Unachjezaji Lyon alafu utegemee kuitwa world class player?
Karim Benzema alikuwepo huko na magoli yake yote lakini hakuwahi kuitwa world class striker mpaka pale alipohamia Real Madrid. Naachaje kukuita mshambuliaji hatari duniani baada ya kuja Arsenal. Karibu sana Arsenal, World Class Striker, Alexandre Lacanyavuuu. Nina furaha kubwa sana acha nim uite nitakavyo.
Napomuona Lacazette amevalia jezi za Arsenal, nakumbuka wakati Thierry Henry kwa mara ya kwanza anasajiliwa na Arsene Wenger. What a transfer? kila mtu akamuona kuwa hafai lakini mwisho wa siku. Mchele ulijitenga na pumba za chuya. Welcome Arsenal, Lacagoal.
Ubora wako uliokuwa ukiuonyesha Lyon ambayo haina wordl class midfielder na winga. Unashindwaje kuuonyesha maradufu ukiwa hapa Arsenal utakapokutana na kiungo muongomuongo, Mesut Ozil na winga hatari zaidi duniani kwa sasa, Alexis Sanchez. Kwa hakika wakati utatueleza.
Arsenal ilisumbuliwa na nafasi mbili tu zilizofanya kutotwaa ubingwa wa England msimu uliopita. Ilisumbuliwa na beki namba tatu na mshambuliaji wa kati. Naachaje kushangili kwa ujio wako Alexandre Lacakambaa. Kama namba tatu tumempata. Striker naye ametua. Naachaje sasa?
Niliacha kufanya mazoezi baada ya kusikia unakabidhiwa jezi pale Emirates jana. Nilichokifanya ni kitu kimoja. Mbio zangu hali ya kuwa nanuka jasho kwenye kibanda umiza na kuanza kuangalia ujio wako. Mama Chanja wangu alikasirika baada ya kuniona nikiwa kwenye hali ya jasho jingi lakini ilikuwa haina jinsi.
Kama nilikubali kukasirikiwa na Mama Chanja wangu anayenipa kila kila anachostahili kupata mwanaume rijali kama mimi na nikatosheka kwa ajili kuangalia ujio wako. Itakuwaje nitakapokushuhudia unafunga hatrick kwenye mechi ya ngao ya jamii dhidi ya Chelsea pale Wembley? Sihitaji kujibu hilo wacha iwe homework kwa wasomaji wangu.
Umeikuta Arsenal ambayo ina kila aina ya viungo. Arsenal ambayo Alexis Sanchez, Mesut Ozil, FRiyadh Mahrez na Thomas Lemar watasubiri kukulisha mipira wewe mtu mmoja ili ufunge. Sitoshangaa kushuhudia ukifunga magoli 50 au 100 mwishoni mwa msimu wa EPL.
Sihitaji kukuita new Thierry Henry kutokana na rekodi kubwa za dunia alizowahi kuziweka na kuvunja pale England na kwenye timu yake ya taifa. Wacha nitumie muda huu kukuita ‘New Didier Drogba’.
Mshambuliaji ambaye aliwashangaza wengi kutoka na kutumia nguvu nyingi akili kidogo kuhakikisha anaipatia timu yake matokeo chanya. Karibu sana Arsenal, new Didier Drogba. Karibu sana Drogba mpya.
Lacazette….Lacazette….Lacazette. Ninamengi ya kukwambia. Nina majina mengi ya kukuita. Nina kesi nyingi za kuwachongea watu. Ila nahitaji kwanza uanze na Bayern kwenye ICC alafu Chelsea.Man United na Liverpool. Karibu sana Alexandre Lacazette nadhani ndugu yangu Charles Abel atakuwa na furaha kubwa sana baada ya kusikia ujio wako.

No comments