Header Ads

Responsive Ads Here

NAMNA SINGIDA ILIVYOHITIMSHA KWA UFANISI NA KUKABIDHI MWENGE WA UHURU SIMIYU.


ME1
Mkuu wa Mkoa wa Simgoda Dkt Rehema Nchimbi akijiandaa kuukabidhi mwenge wa uhuru kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka, katikati yao ni Mkimbiza Mwenge Kitaifa Bahati Lugodisha akiwa na mwenge wa uhuru.

ME2
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhandisi Jakson Masaka akiukabidhi mwenge wa uhuru kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi mara baada ya kuhitimisha mbio za mwenge wa uhuru kwa halmashauri saba za Mkoa wa Singida, ili aweze kuukabidhi mkoa wa Simiyu.
ME3
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akiupokea mwenge wa uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Mkalama kabla ya kuendelea na itifaki ya kuukabidhi kwa mkoa wa Simiyu.
ME4
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt Angelina Mageni Lutambi akiwa na mwenge wa uhuru kabla ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi kuendelea na itifaki ya kuukabidhi kwa mkoa wa Simiyu
ME5
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akisoma taarifa ya mbio za mwenge wa uhuru Mkoani Singida kwa Mwaka 2017 kabla hajaukabidhi kwa Mkoa wa Simiyu, kushoto kwake ni Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa Amour Hamad Amour.
ME6
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akiagana na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa Amour Hamad Amour kabla ya kukabidhiwa Mkoani Simiyu.
ME7
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa Amour Hamad Amour ‘akinyakua’ pamoja na askari wa Mkoa wa Singida kama ishara ya kuagana kwa upendo kabla ya kukabidhiwa Mkoani Simiyu.
ME8
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa Amour Hamad Amour akiwa na wakimbiza mwenge kitaifa kwa pamoja ‘wakinyakua’ pamoja na askari wa Mkoa wa Singida kama ishara ya kuagana kwa upendo kabla ya kukabidhiwa Mkoani Simiyu.
ME9
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Debora Mgiligimba akiongoza askari wengine kuwaaga wakimbiza mwenge kitaifa waliofanya kazi nzuri mkoani Singida katika halmashauri saba.
ME10
Mkuu wa Mkoa wa Simgoda Dkt Rehema Nchimbi akijiandaa kuukabidhi mwenge wa uhuru kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka, katikati yao ni Mkimbiza Mwenge Kitaifa Bahati Lugodisha akiwa na mwenge wa uhuru.

No comments