Header Ads

Responsive Ads Here

Naibu Waziri Anthony Mavunde afunga Mafunzo ya Elimu ya Nyuki Kisaki wilaya ya Singida mjini


 VUD1
Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde akipata maelezo kutoka kwa Ndg Philemon Kiemi mfugaji wa nyuki kutoka Kijiji cha Kisaki,Kata ya Kisaki,Wilaya ya Singida Mjini.


……………………………………………………………………………………

Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde  leo amemtembelea Kijana Mjasiriamali na Msomi aliyebobea katika masuala ya Nyuki na Asali Ndg Philemon Kiemi katika Kijiji cha Kisaki,Kata ya Kisaki,Wilaya ya Singida Mjini.
Pamoja na ziara hiyo pia amepata nafasi ya kujifunza tabia na aina za Nyuki na kutembelea kiwanda chake cha kutengeneza Asali ambapo amewaajiri zaidi ya Vijana 42.
ametumia siku hii pia kufunga Mafunzo ya Elimu ya Nyuki kwa wahitimu waliomaliza mafunzo yao ya miezi mitatu na pia kuweka jiwe la Msingi la Shule ya Elimu ya Nyuki anayoitazamia kuipanua na kuiboresha kukidhi mahitaji ya dunia ya leo katika utoaji hiyo ya huduma ya Elimu.
Waziri Mavunde amemuhakikishia Ndg Philemon Kiemi kumpa ushirikiano wa kutosha kutoka serikalini ikiwa ni pamoja na kumuunganisha na mifuko ya Uwezeshaji wananchi kiuchumi ili apate fedha zaidi za kutanua biashara zake na kutoa fursa zaidi za Ajira kwa Watanzania.

No comments