Header Ads

Responsive Ads Here

NAIBU SPIKA DK. TULIA AKSON AANZA ZIARA YA SIKU KUMI MKOANI MBEYA


Naibu Spika Dr. Tulia Ackson kupitia Taasisi yake ya Tulia Trust ameanza ziara ya siku 10 mkoani Mbeya kazi kubwa ikiwa ni kutoa misaada kwa Taasisi mbalimbali zikiwemo shule na hospitali huku akikagua maendeleo ya baadhi ya Taasisi alizozisaidia katika siku za nyuma.

Dr. Tulia katika ziara yake ya leo alikabidhi misaada vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya Tsh. 1.1m kwa Shule ya Msingi Lubwe,  Tsh. 2.5m kwa Shule ya Sekondari Nkunga, vitanda 20 kwa Hospitali ya Igongwe pamoja na kukagua ujenzi wa Vyoo na Bafu kwa wajawazito katika Hospitali ya Makandana.
MTO1
Naibu Spika Dr. Tulia Akson akiwa amembeba mmoja wa watoto yatima katika Hospitali ya Igogwe
MTO2
Naibu Spika Dr. Tulia Akson akivuka Daraja la Nkunga-Lupepo lililopo Rungwe
MTO3
Naibu Spika Dr. Tulia Akson akisoma moja ya bango lililowekwa na wananchi wakati wa ziara yake
MTO4
Naibu Spika Dr. Tulia Akson akiwa kwenye picha picha ya pamoja na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Rungwe
MTO5
Naibu Spika Dr. Tulia Akson akisalimiana na wazazi katika Hospitali ya Igogwe ambayo haina eneo la kupumzikia wakinamama baada ya kujifungua

No comments