Header Ads

Responsive Ads Here

MTOTO WA MIAKA MINANE AFANYIWA UKATILI KWA KUCHOMWA NA KIJIKO CHA MOTO GEITA


Mtoto huyo akionesha majeraha ya kuchomwa na kijiko ambacho kilikuwa kimepashwa moto maeneo ya miguuni.

Jeraha la Masikioni ambalo na lenyewe alichomwa na mama wa Kambo.


Bi,Benitha Agustine  ambaye ni mama wa Kufikia wa Mtoto ambaye amekuwa akimfanyia ukatili.

Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Esnath Magoti  akizungumzia matukio ya ukatili ambayo yapo Mkoani Humo.


Na Joel Maduka wa Maduka Online.

Vitendo vya
ukatili dhidi  ya watoto bado vimeendelea
kushamiri Mkoani Geita ambapo Kuanzia mwezi Januari hadi  Juni mwaka Huu Jumla  ya makosa ya vitendo vya ukatili dhidi ya  watoto
mia moja Tisini na Tisa (199) vimekwisha ripotiwa kwenye dawati la
Jinsia na Watoto.
 
Akizungumza
na Waandishi wa Habari kwenye  ofisi za
polisi Mkoani Humo,Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Esnath Magoti ,amefafanua
kuwa  mchanganuo wa Makosa hayo ni kesi
za ubakaji,ulawiti ,watoto kutelekezwa ,wengine kutokuwapeleka shule na vitendo
vingine vya ukatili dhidi ya watoto.
 
“Unyanyasaji
wa Kijinsia bado  ni tatizo kubwa sana kwenye Mkoa wetu wa Geita
kwani hadi sasa Jumla ya Kesi mia moja Tisini na Tisa (199) zimekwisha Kufika
kwenye meza yetu na kesi nyingi unakuta ni za ubakaji ,ulawiti na wengine
wanatenda ukatili wa kuwadhuru watoto mara nyingi kesi hizi zinakwama kutokana
na jamii kushindwa kuwa na ushirikiano kwa kutoa taarifa wengine wamekuwa wakimalizana
wao kwa wao kwenye familia zao hali hii inakwamisha sana jitihada za utetezi wa
watoto ambao wanafanyiwa vitendo vya ukatili”Alisema Magoti.
Hata hivyo
kutokana  na juhudi za utoaji wa elimu
juu ya watu kuachana na vitendo vya ukatili hali bado sio swari ambapo kwenye
mtaa wa Msalala Road kata ya Kalangalala,Mama wa kufikia  ambaye anajulikana kwa jina la Benitha
Augustine,amemchoma  mtoto mwenye umri wa
miaka minane (8)  sehemu mbali mbali za
mwili wake na kijiko ambacho alikuwa amekipasha moto kwa madai kuwa alikuwa
akimhadhibu .
 
Akizungumza
na Mtandao wa Maduka Online Jirani wa Mama Huyo Bi,Habiba Rajabu alisema kuwa
Mama Huyo amekuwa na tabia ya kumpiga mara kwa mara mtoto huyo bila sababu hali
ambayo wao kama majirani wamekuwa wakijiuliza labda kwasababu sio mtoto wake wa
kuzaa ndio maana amekuwa akimsulubu kwa mateso ya namna hiyo.
 
 “Sisi kama majirani tumeendelea kumshauri kama
mtoto amemshinda ni bora akampeleka kwa mama yake kuliko kuendelea kumfanyia
vitendo vya ukatili wa  namna hiyo amefikia
hatua hadi anamchoma na kijiko ambacho amekipasha moto kiukweli inaumaa sana
kwa mtoto ambaye ni kiumbe wa Mungu kufanyiwa ukatili wa namna hii yani hadi na
baba yake mzazi ana mapenzi na mtoto ukimkuta anamwadhibu utadhani anaadhibu
jambazi jamani watu tubadilike ukatili wa jinsi hii haukubaliki kwenye jamii
zetu”Alisema Bi Habiba.
 
Aidha mama
Huyo Bi,Benitha Agustine amekiri kufanya kitendo cha kumpiga mwanae na kumchoma
kwa kutumia kijiko ambacho amekichemsha kwenye moto na kwamba amekuwa akifanya hivyo
kutokana na hasira ambazo zinasababishwa na ugomvi baina yake na mume wake
kwani amekuwa akimpiga mara kwa mara hali ambayo imekuwa ikipelekea kupatwa na
hasira ambazo zimekuwa zinapelekea kumwadhibu mtoto wake.
 Kutokana na kufanyiwa ukatili huo Mtoto
huyo   ameiomba serikali kumchukulia
hatua za kisheria mama yake wa kambo kwani imekuwa ni destulri yake kumtesa kwa
muda mrefu hali ambayo imemsababishia kuwa na majeraha sehemu nyingi za mwili
wake.
 
Shida Mpondi
ni Katibu wa Mbunge wa viti maalum Chadema Mkoani Hapa ametoa wito kwa
wazazi,walenzi na baadhi ya watu wenye tabia za namna hiyo kuachana nazo kwani
zinawakosesha haki za msingi watoto na kuwafanya kudumaa kiakili.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE

No comments