Header Ads

Responsive Ads Here

MTOTO WA KIUME AOKOTWA MZAMBARAUNI MKOA WA KASKAZINI PEMBA


PEMB
Na Masanja Mabula -Pemba ..
MTOTO mchanga wa kiume mwenye umri wa siku tatu ameokotwa akiwa ametupwa kwenye kichaka huko katika shehia ya mzambarauni wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba .
akizungumza na gazeti hili   washuhuda wa tukio hilo wamesemawakiwa wanaendelea na shuhuli zao wa kilimo walisikia sauti ya mtoto kwenye kichaka karibu na shamba yao.
Mmoja wa mashuhuda hao Juma Haji Kombo amesema baada ya kufika kwenye kichaka walimkutwa mtoto huyo akiwa amefungwa ndani ya kipolo cha saruji huku akiwa ameziongwa zongwa maguo machafu pamoja na kuitiwa matambara mdomoni .

Juma amezidi kueleza kwamba akiwa na mke wake walichukua hatua za kumtoa mtoto huyo ndani ya polo hiyo na kasha kumsafisha kabla ya kuchukua hatua ya kumpeleka kwa sheha kwa hatua zaidi za kiserikali .
“Mtoto huyo tumemkuta akiwa ndani ya polo la saruji akiwa ametiwa matambara mdomoni na baada ya kumsafisha tulimfikisha kwa sheha wa shehia kwa hatua za kiserikali zaidi ”alifahamisha.
Naye mkuu wa wilaya ya wete Rashid Hadid Rashid ameelezea kusikitishwa na matendo ya udhalilishaji kuendelea kuripotiwa katika wwilaya ya kusema Serikali ya wilaya inaendelea kuchukua hatua za makusudi kuwaelimisha wananchi kupinga matendo hayo
Mkuu wa wilaya amefahamisha kwamba  taarifa za kuokotwa kichanga hicho amezipiokea kutoka kwa sheha na kuagizwa kupelekwa hospitali kwa ajili ya hatua za kiafya .
taarifa zaidi zinasema kwamba tayari jeshi la polisi linamshikilia Hadia Ali Mbarouk anayekisiwa kuwa na umri wa miaka 35  akihusishwa na kitendo cha kumtupa mtoto huyo .
awali katika mahojiano yake na jeshi la Polisi  mtuhumiwa huyo amekana kuhusika na kitendo hicho na baada ya kufanyiwa uchunguzi zaidi akakiri kujifungua mtoto huyo na kisha kumtupa kichakani kutokana na sababu  za ukali wa mama yake .
“Nimejifungua kwa kipindi cha siku tatu , lakini niliamua kumtupa kutokana na ukali wa mama yangu ”alisema.
Taarifa zaidi zinasema kwamba mtuhumiwa anawatoto zaidi ya watatu na kwamba mimba ya mtoto huyo aliyemtupa alipewa na msaani mwenzake ambaye walikuwa wakifanya michezo ya kuigiza pamoja
hali ya afya kwa mtoto huyo inaendelea vyema  baada ya kupatiwa huduma na madaktari wa hospitali hiyo .

No comments