Header Ads

Responsive Ads Here

MTAALAMU WA KILIMO NA MIFUGO AANZA HATUA YA KUACHANA NA UKAPERA AMVIKA PETE MCHUMBA WAKE NA KUTOA MAHARI

 Mtaalamu wa Kilimo na Mifugo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Waco Langu General Supplies Ltd, Humphrey Urine akimvika pete mchumba wake Milkajene Sangiwa ikiwa ni hatua za kwanza kujiandaa kuachana na ukapera katika hafla iliyofanyika nyumbani kwa wazazi wa mchumba wake huyo mjini Morogoro jana. Pamoja na kumvalisha pete tukio la utoaji mahari lilifanyika kwa kushuhudiwa na ndugu wa pande zote mbili. Bibi harusi ni mfanyakazi wa Idara ya Misitu Wilayani Lushoto mkoani Tanga.

 Wachumba wakiwa na wazazi wao wa kike. Kushoto ni Mama wa Bibi harusi mtarajiwa na anayefuatia ni mama wa Bwana Harusi mtarajiwa, Happyness Uromi. Hakika wamependeza na watoto wao. Big Up Humphrey kwa uamuzi huo wa busara ambao umekujengea heshima katika familia hizo mbili.
 Hapa ni picha ya pamoja baada ya matukio hayo mawili ya kumvalisha pete na utoaji wa mahari.
 Hapa ni Humphrey na mama mkwe wake wakionesha upendo 
kwa kukumbatiana.
 Bwana harusi mtarajiwa akifanya mazungumzo na baba mkwe wake Mzee Sangiwa. Hapo ni busara tu zinamwagika kutoka kwa mzee huyo.
 Dada na kaka wakipongezana kwa tukio hilo.
 Ni furaha tupu hapa 
Hapa pete ikioneshwa kimtindo chezea Milka wewe.

No comments