Header Ads

Responsive Ads Here

Mkuu wa Mkoa Wa Kilimanjaro Mhe Anna Mghwira katika ziara ya kikazi wilayani RomboNa Mwandishi wetu, Rombo

Mkuu wa Mkoa wa  Kilimanjaro Mhe Anna Mghwira Jumatano amefanya  ziara ya kikazi wilayani Rombo , ambapo alianza kwa kukutana na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya hiyo  na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama kabla ya  kufika kituo cha uhamiaji kati ya Kenya na Tanzania upande wa  Holili.

 Aliendelea na ziara ndani ya wilaya kupitia eneo la mpaka wa Kenya na Tanzania linalotajwa kama njia ya panya ya kutorosha magendo na mahindi  toka Tanzania kwenda Kenya.

Ziara yake ilifikia kituo kingine cha uhamiaji kati ya Kenya na Tanzania cha Tarakea na kisha kumalizia ziara yake eneo la msitu wa miti ya kupandwa wa Rongai eneo la Kamwanga. Ziara ilianza saa tatu asubuhi na kumalizika sa kumi na mbili jioni.

Mhe Mkuu wa Mkoa alisisitiza kila Mtumishi kutimiza wajibu wake kwa kuwa na UTU NA UZALENDO.

"...Lazima tumpime mtumishi kwa kila siku amefanya kazi gani katika ofisi yake - tangu mlinzi, mfagizi hadi afisa wa juu. Ni lazima tuwajibike. Watumishi lazima mtambue nafasi zenu, mziheshimu na kujua kuwa kazi na nafasi yako ni kiungo cha nafasi na kazi ya mwenzako..."alisema  Mhe. Mghwira.
 Mkuu wa Mkoa Wa Kilimanjaro Mhe Anna Mghwira akilakiwa na Mkuu wa Wilaya ya Rombo Mhe Agnes Hokororo (kulia) alipowasili kuanza ziara ya kikazi wilayani humo 
 Mkuu wa Mkoa Wa Kilimanjaro Mhe Anna Mghwira akilakiwa na watumishi akiwa katika ziara ya kikazi wilayani Rombo 
 Mkuu wa Mkoa Wa Kilimanjaro Mhe Anna Mghwira akitambulishwa kwa watumishi na Mkuu wa Wilaya ya Rombo Mhe Agnes Hokororo  alipowasili kuanza ziara ya kikazi wilayani humo 
  Mkuu wa Mkoa Wa Kilimanjaro Mhe Anna Mghwira akisaini vitabu vya wageni  alipowasili kuanza ziara ya kikazi wilayani Rombo
 Mkuu wa Mkoa Wa Kilimanjaro Mhe Anna Mghwira akisaini vitabu vya wageni  alipowasili kuanza ziara ya kikazi wilayani Rombo
 Mkuu wa Mkoa Wa Kilimanjaro Mhe Anna Mghwira akiongea na watumishi  alipowasili kuanza ziara ya kikazi wilayani Rombo
 Mkuu wa Mkoa Wa Kilimanjaro Mhe Anna Mghwira akiongea na watumishi alipowasili kuanza ziara ya kikazi wilayani Rombo
 Mkuu wa Mkoa Wa Kilimanjaro Mhe Anna Mghwira akiwa na uongozi wa wilaya tayari kuanza ziara yake ya  kikazi wilayani Rombo
 Mkuu wa Mkoa Wa Kilimanjaro Mhe Anna Mghwira akioneshwa maeneo na Katibu Tawala Bw. Abubakar Asenga wakati wa  ziara ya kikazi wilayani Rombo
 Mkuu wa Mkoa Wa Kilimanjaro Mhe Anna Mghwira akitembezwa maeneo mbalimbali katika  ziara ya kikazi wilayani Rombo
Mkuu wa Mkoa Wa Kilimanjaro Mhe Anna Mghwira akiongea na wafanyabishara na wananchi katika ziara ya kikazi wilayani Rombo.

No comments