Header Ads

Responsive Ads Here

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM MH. PAUL MAKONDA AKUTANA NA WAKANDARASI WA WANAOJENGA RELI YA SGR


index
Wakandarasi Wakuu, pamoja na Washauri wa Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kiwango cha Kimataifa (Standard Gauge Railway) kutoka Kampuni ya YAPI MARKEZ (Uturuki) wamemtembelea Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Paul Makonda na kujadiliana Fursa ambazo Mkoa wa Dar es Salaam utazipata wakati wa Ujenzi wa Mradi.

Akizungumza na Wakandarasi na Washauri wa Mradi huo, ambao utajenga mtandao Mpya wa Reli Ya Kimataifa(SGR) awamu ya Kwanza yenye Urefu wa Km 205 kutoka Dar – morogoro Mhe Makonda kwanza amewataka wakandarasi Hao kuhakikisha wanamaliza Ujenzi wa Mradi kwa Muda wa Miezi 30 kama yalivyo Makubaliano na kusisitiza Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam wenye Ujuzi na uwezo wa kufanya kazi za kitaalamu, pamoja na wale wa kazi za kawaida zaidi ya Elfu mbili Mia tano (2,500) watanufaika wakati wa Ujenzi wa Mradi kuanzia Dar es Salaam.
Mhe Makonda amesema viwanda vilivyoko Dar es Salaam vya kutengeneza Simenti, Nondo pamoja na bidhaa zingine vitanufaika pia na kuwataka Wakandarasi hao kutoa vipaumbele kwa Viwanda na wafanyakazi wa Tanzania.
Mradi wa Reli ya Kimataifa (Standard Gauge Railway SGR) utakuwa na Uwezo wa Kutumia Umeme na Mafuta Aina ya Diesel.

No comments